Choline: Kirutubisho muhimu kwa ubongo wa mwanadamu kinachopuuzwa

Choline: Kirutubisho muhimu kwa ubongo wa mwanadamu kinachopuuzwa

Kiambato hiki kimehusishwa na kuboresha utambuzi na kupunguza wasiwasi, lakini je, unakipata kwa kiwango cha kutosha?

Huenda hujawahi kusikia kuhusu choline hapo awali, lakini tafiti zinaonesha kuwa ni muhimu sana kwa afya yetu katika hatua mbalimbali za maisha.

Choline si vitamini wala madini ni kiambato asilia ambacho ni muhimu sana kwa utendaji mzuri wa mfumo wa neva wa binadamu.

Sasa kuna ushahidi unaoibuka kuwa ulaji zaidi wa choline unaweza kuwa na athari mbalimbali zenye nguvu, ikiwa ni pamoja na kuboresha uwezo wa kiakili hadi ulinzi dhidi ya matatizo ya maendeleo ya neva kama vile ADHD (ugonjwa wa kutokuwa na utulivu) na dyslexia (tatizo la kutoweza kusoma vizuri).

Kirutubisho hiki pia kinaonekana kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya neva kwa binadamu. Katika utafiti mmoja, watoto wa mama aliyetumia virutubisho vya choline wakati wa ujauzito walionesha kuwa na kasi ya juu ya uchakataji wa taarifa, kipimo cha ufahamu mzuri.

Wanasayansi wanasema kuwa choline ni kirutubisho cha ajabu, lakini kimekuwa kikipuuzwa sana. Sasa swali ni: choline hupatikana wapi, na je, unakipata kwa kiwango kinachohitajika?

Kirutubisho muhimu

Kila seli katika mwili wetu ina choline, anasema Xinyin Jiang, profesa wa sayansi ya afya na lishe katika Chuo cha Brooklyn huko New York, Marekani.

Choline ni kirutubisho “muhimu”, ambacho inamaanisha tunahitaji kwa afya yetu, lakini miili yetu haitoi vya kutosha ikiwa peke yake. Badala yake, tunahitaji kupata baadhi yake kutoka kwenye mlo wetu.

Kwa maana hii, ni sawa na asidi ya mafuta ya omega 3, ingawa inahusishwa kwa karibu na vitamini B, anasema Emma Derbyshire, mwandishi wa sayansi na mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ushauri la Nutritional Insight.

Choline inaweza kupatikana zaidi katika vyakula vinavyotokana na wanyama, ikiwa ni pamoja na nyama ya ng’ombe, mayai, samaki, kuku na maziwa, lakini pia katika karanga, maharagwe mekundu, uyoga na mboga za cruciferous kama vile broccoli , ingawa vyakula vya wanyama huwa na choline zaidi kuliko vyanzo vya mimea.

Tunahitaji choline kwa kazi nyingi katika miili yetu, pamoja na utendaji kazi wa ini. Ukosefu wa kiambato cha kutosha unaweza kusababisha shida kadhaa.

“Choline husaidia kusafirisha mafuta kutoka kwenye ini, na wakati mtu ana upungufu, anaweza kupata ini yenye mafuta,” anasema Jiang.

Maharage ya soya yanaweza kutoa chanzo kikubwa cha mmea cha choline, ch 120mg kwa 100g.

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Maharage ya soya yanaweza kutoa chanzo kikubwa cha mmea cha choline, ch 120mg kwa 100g.

Choline pia husaidia mwili kuunganisha phospholipids, ambayo ni sehemu kuu ya utando wa seli katika miili yetu. Upungufu wa virutubishi unaweza kuathiri mfumo wa jeni unaohusika katika mchakato wa seli zetu kujitengeneza.

Wakati wa ukuaji wa kijusi (fetus), upungufu wa choline unaweza kuwa na madhara hasa kwa sababu huzuia kuenea kwa seli katika ubongo.

Jukumu la Choline katika ubongo ni muhimu, kwa kweli kimsingi ni “kirutubisho cha ubongo”, anasema Derbyshire. Inahitajika kwa miili yetu kuzalisha neurotransmitter asetilikolini, ambayo ni kemikali ambayo hubeba ujumbe kutoka kwenye ubongo wako hadi kwenye mwili wako kupitia seli.

Asetilikolini ina jukumu kubwa katika seli za neva za ubongo, ambazo zinahitajika kwa ajili ya kumbukumbu yetu, kufikiri na kujifunza.

Katika utafiti mmoja uliohusisha karibu watu 1,400 wenye umri wa miaka 36 hadi 83, watafiti waligundua kwamba watu wenye ulaji wa kiasi cha juu wa choline walikuwa na kumbukumbu bora, na kwamba ulaji wa choline unaweza kusaidia kulinda akili zetu.

Choline kwa kawaida hujumuishwa kama kiungo katika virutubisho vinavyochukuliwa kama “nootropics”, kikundi tofauti cha dutu ambazo watu wengine wanaamini kuwa zinaweza kuboresha kujifunza na kumbukumbu.

Kwa upande mwingine, upungufu wa choline pia umehusishwa na matatizo ya neurodegenerative kama vile ugonjwa wa Alzheimer (kupoteza kumbukumbu) na Parkinson.

Njia nyingine ya choline inaweza kuathiri ubongo ni afya yetu ya akili. Utafiti mmoja uligundua kuwa ulaji wa kiasi cha juu cha choline ulihusishwa na viwango vya chini vya wasiwasi. Katika utafiti mwingine, kuwa na ulaji wa juu wa chakula cha choline kulihusishwa na hatari ndogo ya unyongovu.

Kuwa na ulaji wa kutosha wa choline kunaweza pia kuja na faida nyingine kadhaa.

Kando na hayo, utafiti katika panya umegundua kuwa choline inaweza kusaidia kupunguza viwango vya homocysteine, asidi ya amino ambayo inaweza kuongeza hatari ya ugonjwa wa moyo.

Viwango vya juu vya homocysteine ​​vinaweza pia kuhusishwa na osteoporosis, na utafiti umegundua kwamba watu wenye ulaji wa juu wa choline kutoka kwenye mlo wao huwa na uzito mkubwa wa mfupa, kiashiria cha mifupa yenye nguvu, yenye afya na hatari ndogo ya kuvunjika.

“Choline inaweza kuwa na athari dhidi ya kupoteza mifupa,” anasema Oyen Jannike, mtafiti katika Taasisi ya Utafiti ya Marine nchini Norway, ambaye amechunguza uhusiano kati ya choline na afya ya mifupa.

Hii inaweza kuwa kwa kiasi fulani kwa sababu ya homosisteini, anasema, lakini pia kwa sababu choline ni muundo muhimu katika utando wa seli zetu.

Siku 100 za kwanza

Imethibitishwa kuwa miaka miwili ya kwanza ya mtoto ni muhimu kwa ukuaji wao, na kwamba lishe ya mama wakati wa uja uzito na kunyonyesha ina ushawishi mkubwa juu ya hili.

Uchunguzi unaonesha kwamba choline ni muhimu sana kwa ukuaji wa mtoto tumboni. Kwa kweli, watoto huzaliwa na choline mara tatu zaidi ya mama zao, hali ambayo inaonesha jinsi ilivyo muhimu katika hatua hii ya maisha.

Kulingana na utafiti mmoja, watu wanaokula mayai huwa na takribani mara mbili ya ulaji wa choline

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Tafiti nyingi zimegundua kwamba kuwepo choline ndani ya tumbo la uzazi unahusiana na matokeo ya utambuzi wa mtoto, na manufaa yake yanaweza kuendelea kwa miaka mtoto anapokua.

Katika utafiti mmoja, wanawake wajawazito ambao walikula kiwango kikubwa cha choline katika kipindi cha pili cha ujauzito (kutoka wiki ya 13 hadi wiki ya 28) waliendelea kupata watoto waliopata alama za juu kwenye mtihani wa kumbukumbu ya muda mfupi na ya muda mrefu katika umri wa miaka saba.

Utafiti fulani hata unapendekeza ulaji wa choline wa kutosha wakati mwanamke ni mjamzito unaweza kuhusishwa tabia za ADHD katika watoto wao.

Hatahivyo, tafiti kadhaa zinaonesha kuwa wengi wetu hatupati vya kutosha. Utafiti mmoja uligundua kuwa ni 11% tu ya watu wazima wa Marekani hutumia kiwango cha kila siku kilichopendekezwa.

Mayai ni mojawapo ya vyanzo vya lishe vyenye nguvu zaidi vya choline, na kuna wasiwasi kwamba wale wanaochagua kufuata lishe ya vegan wanaweza kuwa hawapati virutubishi vya kutosha, ingawa kuna vyanzo vingi vya mimea na virutubisho vya choline vinapatikana sana katika nchi zilizoendelea.

Utafiti mmoja uligundua kuwa watu wanaokula mayai wana karibu mara mbili ya ulaji wa kawaida wa choline ikilinganishwa na wale ambao hawana, na kusababisha watafiti kuhitimisha kuwa kutumia kiwango cha kutosha cha choline kila siku ilikuwa “ngumu sana” bila kula mayai au kula choline ya nyongeza.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *