Mzozo wa DRC: Takriban wanajeshi watoro 60 wahukumiwa na mahakama ya kijeshi DRC

Mzozo wa DRC: Takriban wanajeshi watoro 60 wahukumiwa na mahakama ya kijeshi DRC

Kesi dhidi ya wanajeshi sitini watoro wa vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) na washirika wawili wa kike imefunguliwa leo.

Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama ya kijeshi ya Butembo mjini Musienene, katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

“Watuhumiwa wanashtakiwa na mahakama ya kijeshi ya Butembo kwa kumkimbia adui, wizi, ubakaji, unyang’anyi na makosa mengine katika maeneo ya Lubero-Centre, Kimbulu na Musienene,” Seros Muyisa, mwandishi wa habari wa eneo hilo ambaye alikuwepo katika kikao hicho, aliiambia BBC.

h

Waasi wa M23 wamekuwa wakiyateka maeneo ya mashariki mwa DRC tangu kuanza kwa mashambulizi makali mwezi Januari.

Wiki iliyopita, waliingia Bukavu, mji wa pili kwa ukubwa mashariki mwa nchi, na kuchukua udhibiti wa ofisi ya gavana.

Kabla ya Bukavu kuangukia mikononi mwa waasi hao, takriban wanajeshi 80 wa Congo na wanamgambo wa Wazelendo walikuwa wamekamatwa na kuzuiliwa katika gereza la mji huo wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Lakini baada ya shambulio la waasi wa M23, wafungwa kutoka gereza la Bukavu walitoroka, wakiwemo wanajeshi, mamlaka imesema.

Walishutumiwa kwa mauaji na uporaji katika maeneo ya Kabare na Bukavu baada ya kuacha mstari wa mbele, Mkoa wa Kivu Kusini.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *