Tazama mubashara kuapishwa kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump

Tazama mubashara kuapishwa kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump

Rais mteule wa Marekani Donald Trump atarejea tena katika Ikulu ya White House baada ya kuapishwa rasmi kuwa rais wa 47 wa taifa hilo leo Jumatatu tarehe 20 Januari.

BBC Swahili inakueletea mubashara matangazo maalum ya kuapishwa kwake kupitia tovuti yetu na kurasa zetu za mitandao ya kijamii, ikiwemo Facebook, Youtube na pia katika Dira ya Dunia Radio na TV.

ssss

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Sherehe ya utambulisho ni nini?

Utambulisho ni sherehe rasmi inayoashiria kumalizika kwa muda wa rais mmoja madarakani na kuanza kwa utawala wa rais mpya.

Sehemu muhimu ya sherehe hizo ni pamoja na rais mteule kukariri kiapo: “Naapa kwa dhati nitatekeleza kwa uaminifu majukumu ya Ofisi ya Rais wa Marekani, na nitafanya kwa uwezo wangu wote, kuhifadhi, kulinda na kutetea Katiba ya Marekani.”

Ingawa alishinda uchaguzi mwezi Novemba, Trump atakuwa rasmi rais wa 47 mara tu atakaposema maneno hayo.

Naye Vance atakula kiapo ili awe makamu wa rais rasmi.

Tukio hilo pia linajumuisha maonyesho ya muziki, hotuba – wakati ambapo Trump atahutubia wapiga kura wake na kueleza malengo yake ya miaka minne ijayo – vilevile gwaride na kucheza.

Unawezaje kutazama sherehe hiyo?

Kwa kawaida kuna mahitaji makubwa ya watu kuhudhuria sherehe hizo. Wajumbe wa Congress hupokea idadi fulani ya tiketi za sherehe, ambazo wanaweza kuzisambaza kwa wapiga kura wao.

Tiketi hizi ni za bure, lakini mara nyingi ni ngumu kuzipata. Wamarekani wanaweza kuwasiliana na wawakilishi wao moja kwa moja kuomba tiketi.

Ikiwa huwezi kuhudhuria ana kwa ana, kuna njia nyingi za kutazama. Ikulu ya White House inaonyesha mubashara sherehe hiyo kupitia runinga.

Ungana nasi moja kwa moja kwa kubofya link itakayowekwa kwenye taarifa hii baadaye leo Jumatatu ili kufuatilia hafla hiyo kutoka Washington DC kuanzia majira ya saa moja usiku saa za Afrika Mashariki.

Nani atahudhuria?

Maafisa wa serikali wapatao 200,000 wanatarajiwa kujitokeza huko Washington DC, na itajumuisha wafuasi wake na wakosoaji wake.

Maseneta wengi wa Marekani na wabunge pia watahudhuria, pamoja na wageni wa utawala unaokuja.

Mbali na Trump, Vance na familia zao, pia rais anayeondoka na makamu wa rais watakuwepo. Hii inamaanisha tutamuona Rais Biden na Makamu wa Rais Kamala Harris – pamoja na wenza wao Jill Biden na Doug Emhoff.

Marais wa zamani na wake wa rais pia mara nyingi huhudhuria katika hafla hiyo. Mwaka huu unatarajiwa kujumuisha George na Laura Bush na Barack Obama, ingawa Michelle Obama hatahudhuria.

Trump alishinda katika majimbo muhimu ikiwemo North Carolina, Georgia, Pennsylvania na Wisconsin ambayo yalimruhusu kupata kura 312 dhidi ya 226 alizopata mpinzani wake Kamala Harris ambazo zilimrejesha kwenye kiti cha urais

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *