Tetesi za soka Ijumaa 17.01.2025 : Man Utd wamekataa ofa ya Garnacho ya pauni milioni 40

Tetesi za soka Ijumaa 17.01.2025 : Man Utd wamekataa ofa ya Garnacho ya pauni milioni 40

Manchester United imekataa ofa ya pauni milioni 40 kutoka kwa klabu ya Italia Napoli kwa ajili ya winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20. (Mirror)

Everton wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Brazil Willian, 36, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Olympiakos mwezi Desemba. (Telegraph)

Manchester City italazimika kulipa pauni milioni 67 kumnunua beki wa Juventus na Italia Andrea Cambiaso, 24, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Gianluca di Marzio)

 Andrea Cambiaso

Borussia Dortmund wameungana na AC Milan kutaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 27. (Florian Plettenberg, Sky Germany)

Arsenal wamekubali masharti binafsi na nyongeza kubwa ya mshahara na kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 25. (Football Transfers)

West Ham na Tottenham wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Uhispania Ansu Fati, 22. (Sport )

Ansu Fati

Real Madrid wana nia ya kumsajili mlinzi wa kati wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 23, msimu wa joto. (Foot Mercato)

Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia imeanzisha tena mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah. (L’Equipe)

West Ham wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Nottingham Forest na Nigeria Taiwo Awoniyi, 27. (Florian Plettenberg)

Taiwo AwoniyiForest itamlenga mshambuliaji wa Brentford na DR Congo Yoane Wissa iwapo Awoniyi ataondoka katika klabu hiyo mwezi huu. (Telegraph)

Dortmund wanavutiwa na winga wa Brentford na Ujerumani Kevin Schade, 23. (Bild)

Atlanta United wametoa ofa ya £15m kwa mshambuliaji wa Crystal Palace Mfaransa Odsonne Edouard, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Leicester City. (Mail)

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *