Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Liverpool kusubiri hadi msimu ujao kumnunua mshambuliaji wa Brighton Joao pedro – kunani?

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Liverpool kusubiri hadi msimu ujao kumnunua mshambuliaji wa Brighton Joao pedro – kunani?

Mpango wa Liverpool kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Brazil Joao Pedro huenda ukalazimika kusubiri hadi msimu wa joto kwani matakwa ya Seagulls kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 yatafanya uhamisho wa Januari kuwa mgumu. (Football Insider),

Paris St-Germain wako tayari kulipa euro 100m (£83m) kumsajili mshambuliaji wa Newcastle United raia wa Uswidi Alexander Isak, 25. (Fichajes.net – in Spanish).

PSG ya Ufaransa pia inatazamia kulipa euro 58m (£48m) kama kifungu cha kutolewa cha Athletic Bilbao kwa winga wa Uhispania Nico Williams – lakini Manchester United na Barcelona pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (El Desmarque – In Spanish)

.

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Nico Williams

Barcelona wamepoteza imani na kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong na inaonekana kuna uwezekano mkubwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kuondoka katika klabu hiyo ya Uhispania. (Relevo – In Spnish)

Leicester City wanapanga mpango wa pauni milioni 8 kumnunua kiungo wa kati wa Argentina Valentin Gomez, 21, kutoka Velez Sarsfield. (Sun)

Newcastle ni moja ya klabu zinazomtaka beki wa Barcelona Eric Garcia, 23, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City anataka kusalia Nou Camp na kupigania nafasi katika kikosi cha kwanza. (Sport – In Spanish)

Crystal Palace wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Benfica Mjerumani Jan-Niklas Beste, 25, mwezi Januari. (Sky Sports Switzerland)

.

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Lamine Yamal

Real Madrid wanamfikiria beki wa kati wa Uhispania chini ya umri wa miaka 21 Rafa Marin, 22, ambaye alifanya mazoezi katika akademi yao ya vijana na kwa sasa anachezea Napoli. (Fichajes.net – in Spanish)

Blackburn Rovers na Burnley wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Sheffield United kutoka Scotland Oli McBurnie, 28, kutoka Las Palmas ya Uhispania. (Sun),

Winga wa Uhispania Lamine Yamal, 17, anakaribia kuongeza mkataba wake na Barcelona hadi 2030. (Nicolo Schira).

Newcastle itamruhusu mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson, 32, kuondoka bila malipo kandarasi yake itakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider)

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *