Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Manchester United kumuuza Marcus Rushford
Manchester United inataka kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Sky Sport Germany)
United walikuwa tayari kumuuza Rashford aliyehitimu katika akademia yao msimu uliopita na sasa wanapokea ofa mpya. (Telegraph – Subscription Required),
The Red Devils pia wanaweza kumuuza Lisandro Martinez ikiwa Real Madrid itaongeza nia yao ya kumnunua beki huyo wa Argentina, 26. (Talksport),
Arsenal wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Serbia mwenye umri wa miaka 24 Dusan Vlahovic kutoka Juventus Januari. (TeamTalk),
Beki wa kati wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33, yuko tayari kusaini mkataba mpya na Liverpool licha ya kukataa ofa ya awali. (Football Insider),
Newcastle United inamfuatilia winga wa PSV Eindhoven wa Ubelgiji Johan Bakayoko, 21, kabla ya dirisha la uhamisho la Januari. (Telegraph – Subscription Required)
Barcelona wanaweza tu kumsajili Dani Olmo msimu wa ujao kucheza La Liga hadi Disemba 31, lakini fowadi huyo wa Uhispania, 26, atakuwa mchezaji huru ikiwa Barca hawatamsajili tena Januari. (Mundo Deportivo – In Spanish),
Arsenal wana hamu ya kumsajili Dan Ashworth kama mkurugenzi wao mpya wa michezo baada ya kuondoka Manchester United. (ESPN)
Mazungumzo ya Liverpool kuhusu mkataba mpya na mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 32, yanaendelea huku pande hizo mbili zikikaribia kuafikiana kuhusu muundo mpya wa malipo. (Sky Sports),
AC Milan wako tayari kumruhusu nahodha Theo Hernandez kuondoka katika klabu hiyo lakini watadai ada ya takriban £41m kwa beki huyo wa kushoto wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27. (Calciomercato – Itali),
Chelsea haitafikiria kumruhusu mlinzi wa kati Tosin Adarabioyo mwenye umri wa miaka 27 kuondoka kwa mkopo mwezi Januari huku kukiwa na taarifa za yeye kutaka kuelekea West Ham. (Football Insider), nje
Kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 32, anatarajiwa kuondoka Manchester United mwishoni mwa msimu huu. (Fabrizio Romano)
Aston Villa wanafikiria kumwita Louie Barry, 21, kutoka kwa mkopo katika League One Stockport County ili kumpeleka mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye mabao 14 kwa klabu iliyo katika kiwango cha juu zaidi. (TeamTalk),