Jinsi papa Francis atakavyozikwa

Jinsi papa Francis atakavyozikwa

Mazishi ya Papa Francis yatafanyika Vatican Jumamosi, Aprili 26.

Makumi kwa maelfu ya watu, ikiwa ni pamoja na viongozi wengi wa dunia, wanatarajiwa kuhudhuria.

Sherehe hiyo itahusisha nini hasa – na itakuwaje tofauti na mazishi ya papa wengine?

Kwa kawaida, ibada ya mazishi ya papa ina sehemu tatu: tangazo la kifo na mkesha katika makao ya papa; kuuaga mwili na ibada ya mazishi katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro.

Mkesha: Makazi ya Papa

Papa Francis alifariki tarehe 21 Aprili saa 7:35 alfajiri kwa saa za huko. Mwili wake ulichunguzwa na daktari mkuu wa Vatikan Andrea Arcangeli, ambaye aliamua sababu ya kifo na kuandika ripoti.

Mwili wa Papa Francis, ukiwa umevalia mavazi meupe, kisha uliwekwa kwenye jeneza la mbao lililowekwa zinki. Jeneza hilo baadaye lilihamishwa kutoka vyumba vya upapa hadi kwenye kasri la makao ya papa, Casa Santa Marta (Nyumba ya Mtakatifu Martha).

Huko, marehemu papa alikuwa amevalia mavazi mekundu ya kiliturujia, kilemba (kifuniko cha jadi cha maaskofu) na pallium (Kitambaa cheupe au skafu na misalaba iliyopambwa iliyovaliwa na maaskofu wakuu na papa).

Camerlengo – kadinali ambaye anahudumu kama mkuu wa Vatican tangu kifo cha papa hadi uchaguzi mpya – Kevin Farrell alisimamia sherehe ya kutangazwa rasmi kwa kifo cha papa.

Siku mbili baada ya kifo cha Francis, Jumatano, Aprili 23, mwili wake ulihamishwa ukiwa kwenye sanduku wazi kutoka kanisa la Casa Santa Marta hadi kwenye kanisa kuu la Kanisa Katoliki, Basilica ya Mtakatifu Petro.

Huko, kwa muda wa siku tatu, waumini na waombolezaji wanaweza kutoa heshima zao kwa Baba Mtakatifu Francisko.

.

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maandamano hayo kutoka katika makazi ya Papa hadi Kanisa kuu la Mtakatifu Petro yanaambatana na Litania ya Watakatifu wote.

Ibada ya Mazishi: Saint Peters square

Mazishi ya Papa Francis yatafanyika Jumamosi, Aprili 26.

Jioni kabla ya mazishi, saa 8:00 mchana wakati wa Vatican, Camerlengo atasimamia uwekaji muhuri wa jeneza, mbele ya makadinali wengine wa vyeo vya juu.

Uso wa Papa utafunikwa kwa pazia jeupe la hariri, na sarafu zilizochongwa wakati wa upapa wake na orodha ya matendo ya Francis yatawekwa kwenye jeneza.

Mazishi: Santa Maria Maggiore

Baada ya mazishi, jeneza la Francis litapelekwa katika kanisa la Santa Maria Maggiore, mojawapo ya makanisa manne ya papa wa Roma. Iiko nje ya Vatikan upande wa pili wa Mto Tiber.

Papa aliomba katika wosia wake azikwe huko Santa Maria Maggiore. “Siku zote nimekabidhi maisha yangu, huduma yangu ya kipadre na kiaskofu kwa Mama wa Bwana Wetu, Maria Mtakatifu Zaidi,” Papa alieleza.

Alionyesha ni sehemu gani ya basilica anapaswa kuzikwa, na hata akajumuisha mpango.

Francis pia aliomba kaburi lake liwe “kawaida, lisilo na mapambo mengi” na maandishi tu: Franciscus.

Camerlengo Kevin Farrell ataongoza tena mchakato wa mazishi.

Ni akina nani watakaohudhuria mazishi?

Viongozi wengi wa dunia tayari wametangaza nia yao ya kuhudhuria mazishi hayo, kuanzia Rais wa Marekani Donald Trump hadi Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Lakini bado haijajulikana iwapo Zelensky atahudhuria kuagwa kwa baba yake siku ya Jumamosi.

Siku ya Alhamisi, alilazimika kufupisha ziara yake nchini Afrika Kusini kutokana na mashambulizi makubwa ya Urusi.

Vladimir Putin, kama katibu wake wa vyombo vya habari Dmitry Peskov alivyosema, hatakwenda Vatican. Urusi itawakilishwa na Waziri wa Utamaduni Olga Lyubimova.

Makumi – au mamia – ya maelfu ya waumini wanatarajiwa kukusanyika huko Roma.

Takriban watu 50,000 walihudhuria mazishi ya Benedict XVI (aliyekufa baada ya kuacha upapa) mnamo 2023, na takriban 300,000 walihudhuria mazishi ya Papa John Paul II mnamo 2005.

Nani analipia mazishi?

Wosia wa Francis unasema kuwa gharama zote zinazohusiana na mazishi yake zitagharamiwa na mfadhili asiyejulikana. Kiasi chote kitahamishiwa moja kwa moja kwa Basilica ya Santa Maria Maggiore.

Je, mazishi haya yana tofauti gani na yale ya awali?

Ibada zinazohusiana na mazishi ya papa zimeelezewa kwa kina katika Ordo Exsequiarum Romani Pontificis (Tambiko la Mazishi ya Papa wa Kirumi).

Toleo la kwanza la sheria liliidhinishwa na Papa John Paul II mnamo 1998 na kuchapishwa mnamo 2000. Ni toleo hili ambalo lilitumika baada ya vifo vya John Paul II na Benedict XVI.

Hata hivyo, Papa Francis, ambaye alipata fursa adimu ya kutazama mazishi ya mtangulizi wake kama papa, aliomba mabadiliko ya maandishi.

.

CHANZO CHA PICHA, ALBERTO PIZZOLI/AFP VIA GETTY IMAGES

Toleo jipya, lililorahisishwa liliidhinishwa na kuchapishwa mnamo 2024.

Mabadiliko makuu:

  • Sherehe ya kutangaza kifo inayosimamiwa na Camerlengo sasa inafanywa katika kanisa, na si katika vyumba ambako papa alikufa;
  • Mwili wa papa huwekwa mara moja kwenye jeneza;
  • Badala ya majeneza matatu yaliyowekwa ndani ya mingine (yaliotengenezwa kwa mbao ya cypress), kuna jeneza la mbao na zink;
  • Awali wili wa papa aliyekufa ulionyeshwa kwa waombolezaji kwenye gari la maiti na bila jeneza, sasa unaonyeshwa bila gari la kubeba maiti na katika jeneza lililo wazi;
  • Sheria hizo zinaeleza nini cha kufanya ikiwa papa anataka kuzikwa mahali pengine mbali na Basilica ya Mtakatifu Petro.

Nini kinafuata?

Mazishi na mazishi ni siku ya kwanza tu ya kipindi cha maombolezo katika Kanisa Katoliki la Roma linaloitwa novemdiales. Itachukua siku tisa.

Na baada ya hapo, mkutano unaitishwa ili kumchagua papa mpya.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *