Doue: Mchezaji chipukizi wa PSG anayezungumziwa sana Ulaya

Wakati Desire Doue alipotoka polepole baada ya dakika 64 pekee katika uwanja wa Arsenal mwezi Oktoba, kijana huyo alionekana mwenye kipaji cha dhahabu.
Kwa mtu ambaye jina lake linatafsiriwa kuwa zawadi {‘desire gifted’} kwa Kiingereza, kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 ameonyesha umahiri wa majina yake yote mawili kwa kuweka nyuma na kusahau mwanzo wake uliokumbwa na utata.
Hatahivyo Doue alikatishwa tamaa baada ya PSG kupoteza 2 -0 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates katika jedwali jipya la ligi ya mabingwa Ulaya.
Lakini tangu wakati huo amekomaa na kuwa sehemu ya kiungo cha kati ya timu mpya ya PSG iliokusanywa na kocha Luis Enrique , akifanya vyema wakati Manchester City ilipochapwa 4-2 katika uwanja wa Parc des Princes mwezi Januari, akionyesha picha nzuri kama mchezaji wa akiba kabla ya kufunga penalti ya mwisho katika ushindi wa mikwaju ya penalti kwenye uwanja wa Anfield katika hatua ya 16 bora.
Macho yote sasa yataelekezwa kwa Doue kwenye Uwanja wa Villa Park siku ya Jumatano, mmoja wa vijana mahiri – pamoja na kijana gwiji kutoka Georgia Khvicha Kvaratskhelia – wanapoondoka kwenye kile kinachoitwa enzi za’Bling Bling’ za Zlatan Ibrahimovic, Neymar, Kylian Mbappe na Lionel Messi na kufuata maadili ya timu.
Doue ambaye ni mzaliwa wa Angers amepanda ngazi polepole kwani hakuwa akianzishwa katika klabu ya Rennes msimu uliopita kabla ya kuhamia PSG kwa pauni milioni 43 msimu wa joto wakati timu hiyo ilipojaribu kuziba pengo lililoachwa na mshambuliaji mahiri duniani Kylian Mbappe aliyejiunga na Real Madrid .
Doue anatoka katika familia kubwa ya soka , huku kaka yake Guela mwenye umri wa miaka 22 akicheza kama beki wa kulia wa Strasbourg baada ya kuondoka Rennes, wakati binamu yake Yann Gboho ni kiungo mshambuliaji mwenye kipawa huko Toulouse.
Ana asili ya Ufaransa na Ivory Coast, akiichezea Ufaransa kwa mara ya kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Croatia katika robo fainali ya Uefa Nations League mwezi Machi, ambapo alifunga penalti na kuisaiodia timu yake kufuzu baada ya baada ya mikwaju.
Ndugu yake Guela anaichezea Ivory Coast ambapo amefanikiwa kuiwakilisha mara kadhaa ambapo ameishindi mechi za kimataifa.
Ndugu wote waliimarika chini ya uangalizi wa baba yao Maho, ambaye alishirikiana nao kila siku – kuandaa vipindi vya mafunzo nje ya kazi waliyokuwa wakifanya huko Rennes, na bado ana ushawishi wa busara na thabiti kwenye maisha yao.
Kulikuwa na mshangao mkubwa wakati PSG ilipolipa ada kubwa kwa Doue katika msimu wa joto, lakini Rennes ni hodari katika kuendesha biashara kwani wanakuza vipaji vingi.
Wana historia ya kumuuza mchezaji mwenza wa sasa wa Doue, Ousmane Dembele kwenda Borussia Dortmund, Eduardo Camavinga kwenda Real Madrid na Mathys Tel, ambaye sasa yuko kwa mkopo Tottenham Hotspur, kwenda Bayern Munich.
Arsenal, Chelsea, Spurs, Manchester United na Newcastle United zote zilionyesha nia ya dhati kwa Doue – lakini alipiganiwa kati ya PSG na Bayern.
Mtaalamu wa soka wa Ufaransa Julien Laurens aliiambia BBC Sport: “Pengine PSG ingependa kulipa ada ya takriban £34m na kujaribu kuipunguza, wakati Bayern walitaka kulipa zaidi ya £50m – lakini mchezaji huyo alivutiwa na PSG.
“Ada hiyo ilionekana kuwa ya juu kiasi, kama ilivyokuwa wakati PSG walipolipa £34m kwa Bradley Barcola baada ya miezi sita Lyon, lakini kuna malipo ya ziada, kama ilivyo Uingereza, unapouza kutoka klabu ya Ufaransa hadi klabu nyengine ya Ufaransa.
“Lengo kuu lilikuwa kwamba Luis Enrique na mkurugenzi wa michezo Luis Campos wote walishawishika kumpata nyota bora.
“Doue ana kipaji kikubwa, ana nguvu kiakili na kimwili. Huko PSG, wanasema ana miguu ya wachezaji wa raga kwa sababu nusu ya chini ya mwili wake una nguvu sana.
“Walijua huko Paris ingechukua muda lakini walikuwa tayari. Luis Enrique alifurahi sana kumsajili. Alikuwa mchezaji aliyemtaka. Walijua anaweza kuhitaji nusu-msimu, lakini walikuwa na furaha kusubiri.”

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Licha ya hayo yote, wenyeji wa PSG wamefurahishwa sana na kujitolea na taaluma ya Doue.
“Klabu imefurahishwa sana na kazi yake ya utimamu wa mwili, mazoezi ya viungo,” alisema Laurens.
Ilikuwa vivyo hivyo kwa Rennes, kocha wa zamani Bruno Genesio akisema: “Mbali na uwanjani ana ndoto: rahisi, mtulivu, na akili ya uongozi huku akiendelea kuomba ushauri. Yeye ni mtu asiyejali na mwangalifu katika kazi yake. Tayari ni mtaalamu kichwani.”
Doue aligonga vichwa vya habari kwa mara ya kwanza wakati Ufaransa iliposhinda Mashindano ya Ubingwa wa Ulaya kwa Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 nchini Israel mwaka 2022, kisha akawa kwenye benchi kwenye fainali ya Olimpiki mjini Paris miaka miwili baadaye, akiingia baada ya dakika 77 Ufaransa ilipofungwa 5-3 na Uhispania baada ya muda wa ziada.
Michezo ya Olimpiki bila shaka ilichangia mwanzo wake PSG, kukosa maandalizi ya msimu mzuri, licha ya kunufaika na usimamizi makini wa Luis Enrique – ambaye amefanya kazi binafsi na Doue, na kumtia moyo ..
Ameanza mara tano pekee kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu, akiwa amecheza mechi saba akitokea benchi, na kufunga mabao matatu kabla kuongeza mabao mawili.
Ilikuwa katika uwanja wa Anfield ambapo aliweka alama yake , aliingia uwanjani baada ya dakika 67 na kufanya ukomavu wa kushangaza, akikabidhiwa mkwaju wa penalti ulioisaidia PSG.
Laurens alieleza: “Baba, Maho, ana ushawishi mkubwa katika kila kitu wanachofanya. Baadhi ya familia wanafikiri mwana wao ndiye Cristiano Ronaldo anayefuata, bila kujali chochote kinachoendelea uwanjani, walikuwa na ukweli fulani.
“Baada ya mechi ya Arsenal, ambapo hakuonesha mchezo mzuri, walisema hayuko tayari kwa hatua kubwa ya kupanda ngazi nyingine. Walielewa kwamba alipaswa kufanya kazi ya ziada, alipaswa kukomaa. Walikuwa na uhalisia sana kuhusu kile alichopaswa kufanya.

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES