Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Newcastle yamtaka Nunez, Reds ina matumaini ya kumnasa Isak

Nottingham Forest na Newcastle zote zinavutiwa na mshambuliaji wa Liverpool na Uruguay Darwin Nunez, 25, ambaye kuna uwezekano mkubwa wa akaondoka Anfield. (Teamtalk)
Msako wa Liverpool kumnasa mshambuliaji wa Newcastle United na Sweden Alexander Isak, 25, unazidi kushika kasi. (Givemesport)
Bayern Munich wanajitayarisha kutoa ofa ya kumnunua mlinda lango wa Brighton na Uholanzi Bart Verbruggen, 22. (Telegraph)
Meneja wa Manchester United Ruben Amorim anamlenga winga wa Sporting na Ureno Francisco Trincao, 25, kama sehemu muhimu ya marekebisho ya kikosi chake wakati wa kiangazi. (Sportsport)
Manchester United, Arsenal, Paris St-Germain, Bayer Leverkusen, Real Madrid na Atletico Madrid zote zinamuwania mlinda lango wa Espanyol Joan Garcia, 23. (AS).

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Arsenal, Manchester United, AC Milan na Bayern Munich zote zinamuwania mshambuliaji wa Leipzig Benjamin Sesko, 21, lakini raia huyo wa Slovenia anapendelea kuhamia Ligi ya Premia. (Bild)
Nyota mwingine wa Leipzig anaweza kuwa katika mpango wa kuhamia Old Trafford kwani Manchester United wanavutiwa na kiungo wa kati wa Uholanzi Xavi Simons, 21. (Team talk)

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Aston Villa wanapewa nafasi kubwa ya kupata saini ya winga wa Chelsea na Uingereza Noni Madueke, 23. (Givemesport)
Chelsea na Manchester City ni miongoni mwa klabu zinazofikiria kumnunua mlinda lango wa Roma na Serbia Mile Svilar, 25. (Caught Offside)
Newcastle wametoa video ya matangazo ya uwanja mpya wenye uwezo wa kuchukua watu 65,000 katika Leazes Park ikiwa ni dalili kwamba wanapanga kuondoka St James’ Park. (Guardian)
Collette Roche, afisa mkuu wa uendeshaji wa Manchester United, ameibuka kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya mtendaji mkuu wa Newcastle United. (Telegraph)