Tetemeko la ardhi Myanmar: Tunachojua kufikia sasa

Tetemeko la ardhi Myanmar: Tunachojua kufikia sasa

Tetemeko kubwa la ardhi limepiga katikati mwa Myanmar.Tetemeko hilo la ukubwa wa 7.7 lilisikika maeneo mengine ikiwa ni pamoja na Thailand na kusini-magharibi mwa Uchina.Mamia wanahofiwa kufariki, ingawa ni vigumu kupata habari sahihi.

Tetemeko la ardhi lilipiga wapi?

Kitovu cha tetemeko la ardhi kilikuwa kilomita 16 kaskazini-magharibi mwa mji wa Sagaing nchini Myanmar, katika kina cha kilomita 10 (maili 16), Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani (USGS) lilisema.Huu ni karibu na mji wa Mandalay, mji wa pili kwa ukubwa nchini Myanmar wenye wakazi wapatao milioni 1.5, na takriban kilomita 100 kaskazini mwa mji mkuu wa Nay Pyi Taw.

Ni maeneo gani yaliathiriwa?

Nchini Myanmar, kuna ripoti za barabara kuharibiwa katika mji mkuu pamoja na uharibifu wa majengo kote nchini.Mitetemeko mikali pia ilisikika maeneo mengine ikiwa ni pamoja na Thailand na kusini-magharibi mwa Uchina.

Iilikuwa baya kiasi gani?

Huenda ikachukua muda kabla ya takwimu rasmi za majeruhi kujulikana, lakini mjumbe wa timu ya uokoaji iliyoko Mandalay ameambia BBC kwamba idadi ya waliofariki huko “angalau ni mamia”.

Je, hili inalinganishwaje na matetemeko mengine makubwa ya ardhi?

Tarehe 26 Disemba 2004, mojawapo ya matetemeko makubwa zaidi kuwahi kurekodiwa yalipiga pwani ya Indonesia, na kusababisha tsunami ambayo ilisomba jamii nzima karibu na Bahari ya Hindi.Tetemeko hilo la kipimo cha 9.1 liliua takriban watu 228,000.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *