Tetesi za Soka Ulaya: Liverpool kumbakiza Salah, United yamtaka Branthwaite

Tetesi za Soka Ulaya: Liverpool kumbakiza Salah, United yamtaka Branthwaite

Liverpool inasalia na imani kuwa mshambuliaji wake Mmisri Mohamed Salah, 32, na mlinzi wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33, watasaini kandarasi mpya na klabu hiyo kabla ya msimu wa joto. (FootballInsider)

Manchester United wako tayari kufanya kila linalowezekana kumsajili beki wa Everton na England Jarrad Branthwaite, 22, msimu huu wa joto, lakini mpango huo unategemea kama watafuzu Ligi ya Mabingwa. (Sun)

Aston Villa wana chaguo la kufanya mkataba wao wa mkopo kwa mshambuliaji wa Manchester United na Muingereza Marcus Rashford, 27, kuwa wa kudumu msimu huu kwa pauni milioni 40. (Teamtalk),

Jarrad Branthwaite

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Jarrad Branthwaite

Manchester United inamuwinda kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Ujerumani Felix Nmecha, 24, ambaye wanatarajia kumsajili kwa takriban £40m. (Bild)

Liverpool wanazidisha mbio za kumsaka kiungo wa RB Leipzig na Uholanzi Xavi Simons, 21, ambaye atapatikana kwa takriban euro 80m (£67m) msimu huu wa joto. (Caught Offside),

Newcastle wamemfanya mchezaji wa kimataifa wa Bournemouth na Uhispania Dean Huijsen, 19, kuwa chaguo lao namba moja katika safu ya ulinzi msimu huu. (Sun)

Bournemouth wanataka kumsajili kipa wa Hispania Kepa Arrizabalaga, 30, kwa uhamisho wa kudumu kutoka Chelsea msimu huu wa joto, wakait huo huo wakimtaka pia mlinda mlango wa Liverpool mwenye umri wa miaka 26 na mchezaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland, Caoimhin Kelleher (Telegraph),

Xavi Simons,

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Xavi Simons

Nafasi ya Thiago Motta kama meneja wa Juventus iko kwenye shinikizo ikijadiliwa ndani katika klabu hiyo. (Fabrizio Romano)

Arsenal, Liverpool na Chelsea zote zinatayarisha uhamisho wa mlinzi wa Ajax na Uholanzi Jorrel Hato, 19, lakini watakabiliwa na ushindani kutoka kwa Real Madrid. (Caught Offside)

Liverpool wana uwezo wa kutumia zaidi ya £100m kununua mshambuliaji mpya msimu huu wa joto huku mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 25, akitarajiwa kuondoka. (Football Insider)

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *