Tetesi za soka Jumanne: Chelsea kuongeza kasi katika harakati za kumnasa Mainoo

Tetesi za soka Jumanne: Chelsea kuongeza kasi katika harakati za kumnasa Mainoo

Chelsea wanajiandaa kuongeza kasi ya kumtafuta kiungo wa kati wa Manchester United Muingereza Kobbie Mainoo, 19, huku mashaka yakiongezeka kuhusu utimamu wa muda mrefu wa kiungo wa kati wa The Blues na Ubelgiji Romeo Lavia, 21. (CaughtOffside)

AC Milan wanafikiria kumnunua beki wa kushoto wa Crystal Palace, Tyrick Mitchell, 25, wakati wa majira ya joto wakijiandaa kuondoka kwa beki wa kushoto wa Ufaransa Theo Hernandez, 27. (Teamtalk)

Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City, Kalvin Phillips, 29, anaweza kurejea Leeds msimu huu wa joto baada ya kukaa kucheza kwa mkopo Ipswich. (Sun)

Kalvin Phillips

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Manchester City inamfuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Eduardo Camavinga, 22. (Florian Plettenberg)

Arsenal wanapanga kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 27, kutoka Newcastle. (Football Insider)

Manchester United wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Porto mwenye umri wa miaka 20 kutoka Uhispania Samu Aghehowa, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa cha takribani £84m. (GiveMeSport)

Ademola Lookman anatarajiwa kuondoka Atalanta msimu huu wa joto na mshambuliaji huyo wa Nigeria, 27, yuko tayari kurejea Premier League huku akihusishwa na taarifa za kujiunga na Chelsea na Arsenal. (Team talk)

Liverpool wanatafakari iwapo watamnunua mlinzi wa Brighton na Uholanzi Jan Paul van Hecke, 24. (GiveMeSport)

Al-Riyadh, FC Dallas na Wolves ni miongoni mwa vilabu vinavyoonesha nia ya kumnunua beki wa kati wa England, Michael Keane, 32, ambaye mkataba wake wa Everton unamalizika msimu huu wa joto. (Mail)

Michael Keane

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Everton, Marseille na Sevilla wanavutiwa na mshambuliaji wa Rangers kutoka Morocco Hamza Igamane, 22. (Ekrem Konur)

Fikayo Tomori wa AC Milan bado yuko sokoni baada ya taarifa kuwa nusura ajiunge na Juventus na Tottenham mwezi Januari, na beki huyo wa kati wa Uingereza anapatikana kwa takribani euro 20m (£16.8m). (Calciomercato)

Kiungo wa kati wa Brighton na Sweden Yasin Ayari, 21, anavutiwa na Borussia Dortmund na AC Milan. (Football Insider)

Yasin Ayari

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Marufuku ya Paul Pogba itatamatika wiki hii lakini licha ya kupokea ofa kadhaa, kiungo huyo wa zamani wa Ufaransa, 31, bado hajaamua ni wapi pa kurejea tena baada ya kuondoka Juventus. (L’Equipe)

Mshambuliaji wa Scotland Robbie Ure, 21, atasafiri hadi Sweden ili kukamilisha uhamisho kutoka Anderlecht hadi IK Sirius. (Fabrizio Romano)

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *