Ramadhan 2023: Kufunga ni nini?

Kufunga ni ibada, na kama ilivyo kwa ibada zote, kuna sheria fulani ambazo tunapaswa kuzifuata.
Kufunga ni nini?
Kufunga ni kujiepusha na chakula, vinywaji na kuwa na mahusiano na mwenzi wako kwa makusudi kuanzia alfajiri (wakati wa Alfajiri inapoanza na wakati wa Suhur unaisha) hadi kuzama kwa jua (wakati Magharibi inapoanza).
Je, nitaanzaje kufunga?
Saumu huanza mara tu unapoweka nia ya kufunga na kwa hivyo unaepuka kufanya chochote kinachofungua.
Makusudio hayahitaji kusemwa kwa maneno, wala hakuna Dua ya kuanzisha saumu.
Kwa mfungo wowote ule kando na Saumu za Qada (mfungo uliokosa ambao hufungwa tena baadaye), una muda wote hadi adhuhuri (wakati wa Zawal/Zuhr) kuamua kama unataka kufunga au la.
Maana yake ni kwamba ikiwa mtu atajisikia vibaya na akaamua kutofunga wakati wa Suhur, lakini hakula chochote mpaka kidogo kabla ya Adhuhuri, na akajisikia vizuri na akaamua kufunga, basi funga yao itahesabiwa maadamu sio Qada.
Ikiwa ni Saumu ya Qada, nia lazima itolewe kabla ya Saumu kuanza Alfajiri.
Nani anapaswa kufunga?
Yeyote anayekidhi vigezo vifuatavyo ni lazima afunge:
• Aliyebalehe kufikia wastani wa umri wa balehe wa miaka kumi na nne na nusu katika kalenda ya Gregorian)
• Mwenye akili timamu – mtu yeyote anayesumbuliwa na ugonjwa wa akili ambao ama huwafanya wasijue kufunga, au wasiweze kuelewa wazo la kufunga (kama vile wale wanaosumbuliwa na Down Syndrome) hawatalazimika kufunga.
• Ikiwa si mgonjwa na mwenye magonjwa sugu ambayo huzuia kufunga, kama vile kisukari kali, au hata udhaifu kutokana na uzee.
• Msafiri ambaye haendi safari ya zaidi ya maili arobaini na nane.
• Kufunga hakutamdhuru mtu au mtoto wake (ikiwa mwanamke ni mjamzito au ananyonyesha).
Je, vipi ikiwa mtu anaruhusiwa kutofunga?
Ikiwa mtu kwa kweli anahisi kuwa hapaswi kufunga kwa sababu mbili za mwisho, anapaswa kuthibitishwa na daktari, daktari wa Kiislamu ambaye anaelewa umuhimu wa Kiislamu wa kufunga pamoja na kuangalia afya yako, badala ya kuangalia tu madhara ambayo inaweza kuwa nayo.
Ingawa afya ni muhimu sana kwa vile miili yetu ni amana kutoka kwa Allah Taala, tunapaswa kukubali tu ikiwa tunahitaji – si kwa sababu tu tunaweza kuwa wadhambi vinginevyo, lakini kwa sababu tunapaswa kuhisi kwamba tunakosa malipo na faida nyingi za kufunga.
Ama wasafiri, ingawa wameondolewa, kama wanaweza, wao pia wanapaswa kufunga ikiwa hali si ngumu.
Katika zama za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kusafiri kulihitaji kuvuka majangwa kwenye joto linalowaka kwa muda wa wiki na hatari ya upungufu wa maji mwilini.
Kwa sababu safari imekuwa rahisi, tunapaswa kujaribu kufunga kama tunaweza.
Mwishowe, ingawa watoto ambao sio Baligh wamesamehewa, wao pia wanapaswa kuhimizwa kufunga kutoka kwa umri mdogo ikiwa wako tayari na haiathiri afya au masomo yao.
Mazingira ambayo kila mtu anakula Suhur na Iftar yake pamoja, anaswali Tarawih msikitini pamoja (au nyumbani kwa wasichana na mama zao), pamoja na mawaidha ya mara kwa mara ya malipo ya Allah Taala, yatajenga hisia ya kudumu ya kukumbukwa na watoto ambayo huwafanya wasiishie na Ramadhani tu wakiwa wakubwa, bali waipende pia.
Iwapo mtu hawezi kufunga kwa dhati, atatakiwa kutoa Fidya, ambayo ni kutoa kiasi kilichotolewa kwa ajili ya Sadaqatu’l Fitr kwa kila siku ambayo hawezi kufunga.

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Ramadhani na Quran
Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alipata wahyi wa kwanza wa Surah Alaq katika mwezi wa Ramadhani.
Qurani Tukufu kwa mara ya kwanza iliandikwa na Allah Taala katika Lawh Mahfuz (Ubao Uliohifadhiwa).
Kisha ikashushwa kutoka hapo hadi kwenye mbingu ya chini kabisa katika Laylatul-Qadr, usiku maalum unaopatikana katika mwezi wa Ramadhani.
Hii inaonesha kuwa Qur’ani Tukufu iliteremshwa na Allah Ta’ala katika mwezi wa Ramadhani kwa njia mbili.
Allah Taala aliuchagua mwezi huu uliobarikiwa ili kuteremsha Kitabu Chake Kitukufu, akionyesha jinsi gani mwezi huu lazima uwe muhimu.

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES
Ramadhan katika Hadith
Ikifika Ramadhani, milango ya mbinguni inafunguliwa, na milango ya Jahannam inafungwa, na Mashayatin wanafungwa minyororo.
Mwezi wa Ramadhani unapoingia huwa ni rahisi kuingia mbinguni na kuwa ngumu zaidi kuingia motoni, kwani Allah Taala anarahisisha kufanya mambo ya kheri na kuwa magumu zaidi kufanya madhambi.
Sababu moja ni kwa sababu Shayatin, ambaye kwa kawaida anatuhimiza kufanya dhambi kwa kuweka mawazo ndani ya mioyo yetu, amefungwa minyororo na hawezi tena kutuathiri.
Hili linazua swali: Kwa nini baadhi ya watu bado wanafanya dhambi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani
Wanachuoni wanaeleza kwamba inaweza kuwa ni kwa sababu si Shayatin wote wamefungwa: ni wale tu wabaya zaidi (kama Hadiyth nyingine inavyoeleza).
Au inawezekana tukawa tumezoea kutenda madhambi kwa mwaka mzima hata ikawa ni tabia na uraibu, na tunaona ni vigumu kuyaacha, ingawa hakuna Shayatin wa kutuzushia zaidi ya manufaa ya kiroho ya funga, kuna hata faida za kiafya:
1. Mwili wetu huanza kujirekebisha.
2. Tunapoteza mafuta yasiyotakikana.
3. Hupunguza hatari ya kisukari.
4. Husaidia kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo kwa kupunguza shinikizo la damu, viwango vya cholesterol, na vichochezi vingine vyenye madhara.
5. Husaidia ukuaji wa niuroni mpya katika ubongo wako.
6. Tafiti zinaonyesha inazuia magonjwa kama vile Alzeima na saratani.
7. Huupa mwili wako dawa ya kuondoa sumu mwilini na kutoa sumu hatari zilizopo kwenye mwili wako.
Mwisho, funga hutusaidia kuelewa yale ambayo watu maskini duniani wanapitia, na kuthamini chakula ambacho Allah Taala ametupa.
Hata hivyo, makusudio makuu ya saumu ni yale ambayo Qur’ani Tukufu inatuambia: inatusaidia kukuza Taqwa na nidhamu binafsi ambayo inatuwezesha kujitawala wakati tuna matamanio ya kufanya madhambi.
Kinachovunjika na kubadilisha funga
Kufunga ni kuanzia alfajiri hadi machweo.
Hata hivyo, ikiwa mtu anakula, kunywa au kuwa na uhusiano na mwenzi wake wakati wowote kati ya nukta hizo mbili, saumu yake inaweza kukatika na kuwa batili.
Yafuatayo yanafungua mfungo: • Kula, kunywa kwa makusudi huku ukijua kuwa umefunga.
Hii pia ni pamoja na:
- Kumeza dawa ya meno au ya kuosha kinywa.
- Kumeza damu kutoka kwenye ufizi ikiwa ni zaidi ya mate iliyochanganywa.
- Kumeza mabaki ya chakula katikati ya meno yako ikiwa ni saizi ya mbaazi ndogo au kubwa zaidi.
- Wakati unatumia dawa ya kupita kwenye pua had kwenye koo lako.
- Kuvuta pumzi katika dawa kama vile unapotumia vipumulio vya pampu ya ugonjwa wa pumu.
- Kumeza maji unapovuta mdomo wako.
- Kuvuta moshi kimakusudi, kama vile unapovuta sigara au kuvuta shisha.
- Kuwa na mahusiano na mwenzi wako au kuchochewa kumwaga manii.
- Kutapika kwa mdomo kwa makusudi.
- Kumeza mdomo uliojaa matapishi kwa makusudi, hata kama hutoi nje kwa makusudi.
- Kufanya uchunguzi wa endoskopi (kukaguliwa na kamera iliyopitisha kwenye bomba la chakula).
- Wakati mwanamke anapoanza hedhi au kutokwa na damu baada ya kuzaa kufunga.
- Kula, kunywa au kuwa na mahusiano na mwenzi wako huku ukisahau kuwa unafunga.
- Hata hivyo, ikiwa ulifikiri kwamba mfungo wako umekatika, kisha ukala kwa makusudi. Mfungo wako sasa utakatika
- Kumeza mate yako mwenyewe au unyevunyevu uliobaki mdomoni mwako baada ya kusukutua.