Papa Francis aonesha ‘maendeleo mazuri ‘, asifu ‘huruma’ ya wahudumu wa matibabu

Papa Francis aonesha ‘maendeleo mazuri ‘, asifu ‘huruma’ ya wahudumu wa matibabu

Papa Francis, ambaye amekuwa akiugua homa ya mapafu kwa zaidi ya wiki tatu, aliwasifu wahudumu wa afya wanaomhudumia kwa uangalizi wao “wa huruma”.

Kwa Jumapili ya nne mfululizo, papa wa Argentina hakuwepo kutoa baraka zake za kila wiki, lakini Vatican ilishiriki maandishi yaliyotayarishwa na papa.

“Nikiwa hapa, ninafikiria watu wengi ambao wako karibu na wagonjwa,” Papa alisema, akimaanisha wafanyakazi wa matibabu, akiwaelezea kama watu wenye “kuleta mwanga kidogo katika usiku wa maumivu.”

Vatican ilisema Jumamosi kwamba papa ameonesha “mwitikio mzuri” katika siku za hivi karibuni katika matibabu yake yanayoendelea katika Hospitali ya Gemelli ya Roma.

Francis aliandika kwamba anahisi “kutunzwa kwa busara na huruma, hasa kutoka kwa madaktari na wafanyakazi wa afya, ambao ninawashukuru kutoka moyoni mwangu.”

“Nafikiria watu wengi walio karibu na wagonjwa kwa njia mbalimbali, ambao ni ishara ya kuwapo kwa Bwana,” aliongeza.

“Tunahitaji huu – muujiza wa wema – ambao wale walio katika dhiki wanauhitaji, na ambao huleta mwanga mdogo katika usiku wa maumivu,” aliongeza.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *