Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Real Madrid inavutiwa na Ibrahima Konate

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Real Madrid inavutiwa na Ibrahima Konate

Klabu ya Real Madrid inavutiwa na beki wa Liverpool Ibrahima Konate, 25. (Mail – usajili unahitajika)

Real pia inamtaka beki wa Bournemouth Dean Huijsen, 19, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa na klabu yake akitoa takriban £50m katika kandarasi yake. (Talk sports)

Liverpool inapanga kutoa kitita cha pauni milioni 40 kumsajili beki wa Bournemouth kutoka Hungary Milos Kerkez, 21. (Telegraph – usajili unahitajika)

West Ham iko mbioni kumsajili kiungo wa Uingereza Angel Gomes, 24, kwa uhamisho wa bure kutoka Lille msimu huu wa joto. (Guardian)

Barcelona inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Newcastle Mbrazil Bruno Guimaraes, 27, ambaye pia ananyatiwa na Arsenal na Manchester City. (CaughtOffside)

Kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani Joshua Kimmich, 30, hataki kujiunga na Arsenal kwa uhamisho wa bila malipo msimu huu wa joto ingawa Paris St-Germain pia imeonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Bild – kwa Kijerumani)

Winga wa Manchester United na Brazil Antony, 25, ameelezea nia ya kusalia Real Betis msimu wake wa mkopo katika klabu hiyo ya La Liga utakapomalizika. (Canal Sur, via mail)

Manchester United inawafuatilia mlinda lango wa Burnley Muingereza James Trafford na kipa nambari moja wa Espanyol Mhispania Joan Garcia, 23, kuchukua nafasi ya Andre Onana, 28. (Teamtalk)

Onana

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Liverpool ndio klabu ya hivi punde zaidi kuonyesha nia ya kumsajili Benjamin Sesko wa RB Leipzig. Kuna tetesi kwamba mshambuliaji huyo wa Slovenia mwenye umri wa miaka 21 angependelea kuhamia London, huku Arsenal na Chelsea zikiwa na hamu ya kumsajili . (TBR Football)

Tottenham huenda ikamuuza mchezaji wa kimataifa wa Mali Yves Bissouma, 28, msimu huu wa joto huku wakijitahidi kuimarisha safu yao ya kati (Football Insider).

West Ham wameulizia mshambuliaji wa Roma Muingereza Tammy Abraham, 27, ambaye kwa sasa anakipiga AC Milan kwa mkopo. (Team Talk)

Newcastle ina mpango wa kuwasilisha ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina mwenye umri wa miaka 25, Moise Kean. (GiveMesport)

Everton iko tayari kufikia makubaliano ya kumsajili tena mshambuliaji wa Brazil Richarlison, 27, kutoka Tottenham. (TBR Football)

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *