‘Nchi inakaribia kulipuka kwasababu ya vita’ – Kabila anazungumza baada ya miaka mitano ya ‘ukimya’

‘Nchi inakaribia kulipuka kwasababu ya vita’ – Kabila anazungumza baada ya miaka mitano ya ‘ukimya’

Baada ya takriban miaka mitano ya kuwa kimya kwa kiasi kikubwa katika siasa na vyombo vya habari, Joseph Kabila, rais wa zamani wa DR Congo, ametangaza kuwa nchi hiyo “iko karibu kulipuka kutokana na vita vya ndani” ambavyo vinaweza kuyumbisha kanda nzima.

Félix Tshisekedi, ambaye alimrithi mwaka wa 2019 – katika makabidhiano ya kwanza ya amani ya mamlaka katika historia ya DR Congo – mwezi huu alisema Kabila ndiye “mtu halisi nyuma ya haya yote”, akimshutumu kulisaidia vuguvugu la M23.

Tangu mwaka 2019 Joseph Kabila ambaye ni seneta amekuwa akizungumziwa na msemaji wake Barbara Nzimbi, lakini wiki hii gazeti la Sunday Times la Afrika Kusini lilichapisha maoni ya Bwn. Kabila hukusu mzozo wa DRC.

Alimshutumu Bw Tshisekedi kwa kukiuka mara moja mikataba mipya ya kisiasa ambayo ilikuwa imekubaliwa mara tu baada ya kukabidhiwa madaraka.

Ameongeza kuwa hali “imekuwa mbaya zaidi. Hadi kufikia hatua ambayo nchi iko kwenye hatihati ya kulipuka kutokana na migogoro ya ndani, inaweza hata kuyumbisha eneo lote.”alisema.

g

CHANZO CHA PICHA, AFP

Maelezo ya picha, Tshisekedi (kulia) alimshutumu mrithi wake Kabila (pichani akikabidhi madaraka mwaka wa 2019) kwa kuwa nyuma ya kile kinachoendelea Mashariki mwa DRC

Rais Tshisekedi yuko vitani na vuguvugu la M23, ambalo kwa sasa linadhibiti sehemu kubwa za majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini. Anamtuhumu Kabila, na Rwanda, kuwa nyuma ya M23, na wikendi hii aliahidi kupanga upya jeshi kukabiliana na kundi hilo.

Joseph Kabila alitangaza kwamba “ikiwa migogoro hii na mizizi yake haitashughulikiwa ipasavyo, juhudi za kuimaliza zitakuwa bure”.

Kabila anasema tatizo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo sio tu kuhusu vuguvugu la M23 – anamshutumu Tshisekedi kwa “kujaribu kudhihirisha kulielezea kundi hilo kama la kigeni ambalo halina sababu halali za kupigania”, jambo ambalo sio ukweli.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *