Tetesi za soka Ijumaa 17.01.2025 : Man Utd wamekataa ofa ya Garnacho ya pauni milioni 40
Manchester United imekataa ofa ya pauni milioni 40 kutoka kwa klabu ya Italia Napoli kwa ajili ya winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20. (Mirror)
Everton wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Brazil Willian, 36, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Olympiakos mwezi Desemba. (Telegraph)
Manchester City italazimika kulipa pauni milioni 67 kumnunua beki wa Juventus na Italia Andrea Cambiaso, 24, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Gianluca di Marzio)
Arsenal wamekubali masharti binafsi na nyongeza kubwa ya mshahara na kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 25. (Football Transfers)
West Ham na Tottenham wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Uhispania Ansu Fati, 22. (Sport )
Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia imeanzisha tena mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah. (L’Equipe)
West Ham wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Nottingham Forest na Nigeria Taiwo Awoniyi, 27. (Florian Plettenberg)
Dortmund wanavutiwa na winga wa Brentford na Ujerumani Kevin Schade, 23. (Bild)
Atlanta United wametoa ofa ya £15m kwa mshambuliaji wa Crystal Palace Mfaransa Odsonne Edouard, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Leicester City. (Mail)