Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Liverpool tayari kumuuza Darwin Nunez
Liverpool tayari kumuuza Darwin Nunez, AC Milan wanafikiria kumnunua Marcus Rashford kwa mkopo, na Evan Ferguson ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa wa West Ham.
Liverpool wako tayari kupokea ofa ya pauni milioni 50-60 kumuuza mshambuliaji wao wa miaka 25 wa Uruguay Darwin Nunez. (Football Insider)
AC Milan yaibuka kuwa klabu ya hivi punde kufikiria kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Marcus Rashford, 27. (Mail)
West Ham wanaandaa orodha ya washambuliaji wanaopania kuwasajili Januari hii ikiwajumuisha mshambuliaji wa Brighton wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, mshambuliaji wa Wolves wa Korea Kusini Hwang Hee-chan, 28, na mshambuliaji wa Middlesbrough wa Ivory Coast Emmanuel Latte Lath, 26. (Telegraph – usajili unahitajika)
Mshambuliaji wa Brazil Matheus Cunha, 25, anakaribia kusaini mkataba mpya ulioboreshwa katika klabu ya Wolves licha ya Arsenal kumtaka. (Telegraph – usajili unahitajika)
Randal Kolo Muani huenda akaondoka Paris St-Germain mwezi huu, huku AC Milan, Juventus, Bayern Munich, RB Leipzig, Aston Villa na Tottenham zikimuwania mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26. (Ben Jacobs)
Kiungo wa Chelsea Cesare Casadei amekubali dili la kujiunga na Torino inayoshiriki Ligi ya Serie A, ingawa klabu hivyo vimetofautiana kuhusu ada ya Mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 21. (Gianluca di Marzio).
Galatasaray wana imani “100%” kwamba mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 26, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu hiyo kutoka Napoli, hataondoka Uturuki Januari. (Florian Plettenberg)
AC Milan wamejitolea kumsajili Dani Olmo wa Barcelona kwa mkopo wa miezi sita ingawa mshambuliaji huyo wa Uhispania, 26, hapatikani kwa sasa kutokana na vikwazo vya usajili wa La Liga vilivyowekwa dhidi ya Barca. (Corriere della Sera, via Sport)
Barcelona wamepokea ofa isiyo rasmi kuhusu upatikanaji wake lakini Olmo hana nia ya kuhuama. (Marca – kwa Kihispania)
Klabu ya Santos ya Brazil imewasilisha ombi la kutaka kumsajili kiungo wa Uingereza Josh Windass, 30, kutoka Sheffield Wednesday. (TalkSport)
Swansea City ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya Ulaya vinavyowania kumnunua kiungo wa Saudi Arabia Abdulmalik al-Jaber, 20, anayechezea timu ya Zeljeznicar nchini Bosnia. (TeamTalk)