Angelina Jolie na Brad Pitt wafikia makubaliano ya talaka baada ya vita vya miaka minane mahakamani

Angelina Jolie na Brad Pitt wafikia makubaliano ya talaka baada ya vita vya miaka minane mahakamani

Nyota wa Hollywood Angelina Jolie na Brad Pitt wamefikia makubaliano ya talaka baada ya miaka minane, wakili wake ameviambia vyombo vya habari.

Hapakuwa na maoni ya mara moja kutoka kwa wakili wa Bw Pitt walipombwa kutoa maoni yao, shirika la Associated Press linaripoti.

Wawili hao walifunga ndoa mwaka wa 2014 na wana watoto sita.

Bi Jolie aliwasilisha kesi ya talaka mwaka wa 2016, akitaja “tofauti zisizoweza kusuluhishwa”.

Wawili hao walijiingiza katika malumbano makali ya kulea mtoto katika miezi iliyofuata tangazo la talaka.

Mnamo 2021 hakimu alitoa haki ya pamoja ya malezi ya watoto kwa wazazi wote wawili.

Wanandoa hao walijulikana kama “Brangelina” na mashabiki na waliigiza pamoja kwenye filamu ya 2005 Mr and Mrs Smith.

Ndoa hiyo ilikuwa ya pili kwa Bw Pitt – hapo awali alifunga ndoa na nyota wa Friends Jennifer Aniston – na Bi Jolie ilikuwa ni ndoa yake ya tatu baada ya kuolewa na waigizaji Billy Bob Thornton na Jonny Lee Miller.

Bi Jolie ameigiza katika filamu za Lara Croft: Tomb Raider, Changeling and Girl, na Interrupted huku filamu ya Mr Pitt ikijumuisha Fight Club, Once Upon a Time in Hollywood na Twelve Monkeys.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *