Watu wameanza kufa kwa kiu na njaa huko Mayotte” – Seneta wa Ufaransa
Kufuatia kimbunga cha Chido, seneta wa eneo hilo amemwambia mtangazaji wa Ufaransa kuwa watu “wanaanza kufa kwa kiu na njaa” huko Mayotte.
Akizungumza kutoka shule ambayo imegeuzwa kuwa makazi katika kisiwa hicho, Salama Ramia ameiambia BFM TV: “Kuna wagonjwa. Watu wanalala chini.”
Tovuti ya Mkuu wa Mkoa wa Mayotte ilisema jana kuwa kazi inaendelea kubaini na kurekebisha uharibifu wa maji na usambazaji wa umeme kisiwani humo.
Hiki ndicho kimbunga kibaya zaidi kuwahi kukumba visiwa hivyo katika kipindi cha miaka 90, kikiwa na mawimbi yanayofikia urefu wa mita nane.
Kisiwa cha Mayotte ni sehemu ya milki ya Ufaransa na ni moja wapo ya sehemu masikini zaidi nchini Ufaransa – idadi kubwa ya watu jumla 300,000 wanaishi katika miji duni.