Putin atangaza kunyakua maeneo 189 nchini Ukraine mwaka huu

Putin atangaza kunyakua maeneo 189 nchini Ukraine mwaka huu

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kwamba 2024, askari wa Urusi wameteka maeneo 189 huko Ukraine, ameyasema hayo wakati akizungumza na majenerali wa kijeshi.

Waziri wa Ulinzi Andrei Belousov baadaye aliongeza kuwa kilomita za mraba elfu 4.5 za eneo la Ukraine zimetekwa tangu mwanzo wa vita.

Putin ameamuru vikosi vya nyuklia viwe tayari na amesema uzalishaji wa silaha katika viwanda vya Oreshnik uendelee kwa siku za usoni.

Vilevile, Putin amedai kuwa kwa wastani zaidi ya watu elfu moja wamejiunga na jeshi kila siku mwaka huu, na kusema kuwa nguvu za jeshi la Urusi zimeongezeka hadi wanajeshi milioni 1.5.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *