Norway kutenga dola milioni 240 kuimarisha jeshi la wanamaji la Ukraine

Norway kutenga dola milioni 240 kuimarisha jeshi la wanamaji la Ukraine

Norway itatoa dola za Kimarekani milioni 240, kuimarisha Jeshi la Wanamaji la Ukraine ili kusaidia kuzuia shughuli za kijeshi za Urusi katika Bahari Nyeusi, serikali ya Norway imesema.

“Ukraine inahitaji msaada wa ziada ili kuzuia vikosi vya wanamaji wa Urusi katika Bahari Nyeusi katika siku za usoni. Hili ni muhimu ili kulinda wakazi wa Ukraine na miundombinu ya Ukraine dhidi ya mashambulizi ya Urusi,” AFP inamnukuu Waziri Mkuu wa Norway Jonas Gahr Støre.

“Pia ni muhimu kulinda mauzo ya nafaka na bidhaa nyingine zinazoiletea Ukraine mapato makubwa,” aliongeza.

Pesa hizo zitatumika kununua vifaa, vikiwemo vya kutegua mabomu, pamoja na kuwafunza wanajeshi wa Ukraine.

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *