Kwanini Israel inashambulia Syria?

Kwanini Israel inashambulia Syria?

Israel imefanya mashambulizi ya angani zaidi ya mia moja dhidi ya vituo vya kijeshi vya Syria na pia imepeleka jeshi lake katika eneo lililo na ulinzi mkali mpakani katika eneo la mlima Golan ,ikipanua maeneo ya Syria ambayo yametekwa na Israel.

Israel inasema inachukua hatua hii ili kulinda usalama wa raia wake lakini wenine wanasema ni fursa ya kudhoofisha adui wa muda mrefu.

Je ni mashambulizi ya aina gani ya angani ambayo Israel imekuwa ikiyatekeleza?

Ramani

Shirika la Syrian Observatory for Human Rights (SOHR) lililopo Uingereza limesema limeorodhesha zaidi ya mashambulizi ya anga 310 ya jeshi la ulinzi la Israel (IDF) tangu kuanguka kwa utawala wa Assad Jumapili.

Mashammbulizi hayo yalilenga vitio vya kijeshi vya Syria kutoka Aleppo kaskazini hadi Damascus kusini ,ikiwemo maghala ya silaha ,vituo vya majini na vituo vya utafiti.

Rami Abdul Rahman,muanzilishi wa shirika la SOHR, amesema mashambulizi hayo yamekuwa yakiharibu ”uwezo wote wa vikosi vya Syria” na kusema kuwa ”haki za wasyria zimekiukwa”.

Israel inasema hatua zake ni kuhakikisha silaha hazifikiwa na waasi walio na misimamo mikali wakati Syria iko katika hali ya mpito kutoka kwa utawala wa Assad .

Je,Israel ina wasiwasi gani kuhusu silaha za kemikali?

Shambulio linaloshukiwa kuwa la kemikali huko Douma, karibu na Damascus na vikosi vya pro-Assad mnamo 2018

CHANZO CHA PICHA, AFP

Maelezo ya picha, Shambulio linaloshukiwa kuwa la kemikali huko Douma, karibu na Damascus na vikosi vya pro-Assad mnamo 2018

Israel ina wasiwasi kuhusu ni nani atakayefikia silaha za kemikali zinazodaiwa kuwa za Bashar al- Assad.

Haijulikani ni wapi au kiasi gani cha silaha hizi Syria inazo ,lakini inadhaniwa kuwa rais mstaafu Bashar al- Assad alikusanya akiba ya silaha hizo.

Siku ya Jumatatu, mlinzi wa kemikali wa Umoja wa mataifa alitoa onyo kwa mamlaka za Syria kuhakikisha kuwa silaha hizo ziko salama.

Ake Sellstrom,aliyekuwa mkuu wa wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa nchini Syria,alisema kuwa Israel imelenga uwezo wa Syria wa silaha za kemikali kwa mashambulizi yake ya angani.

“Kile kinachofanywa na Israel ni kuondoa mali,” na kuongeza kwamba mali hizo zinaweza kuwa watu, vituo, au vifaa.

Vikosi vya usalama vinavyoegemea Bashar al-Assad wanajulikana kutumia gesi aina ya Sarin katika shambulizi kwenye kitongoji cha jiji la Damascus kinachojulikana kam aGhouta mwaka 2013,ambayo inamaanika kuua zaidi ya maelfu ya watu.

Pia wanalaumiwa kutumia silaha za kemikali kama vile gesi za Sarin na Chlorine katika mashambulizi ya hivi punde.

Dkt Selltrom anasema vikosi vya waasi huenda wakawa wana akiba ya silaha za kemikali ,kwani wameaminika kutumia silaha hizo awali wakishambulia mahasimu wa Syria.

“Assad amekuwa na silaha hizi za kemikali kama njia moja ya kujipanga kuzidi nguvu Israel,na hawangetumia kabla ya kuchokozwa.Lakini sasa kuna serikali mpya mamlakani.

“Israel itaelekea kuzichukua slaha hizo za kemikali….kile ambacho kimeaminika ni silaha za kemikali.”i

Je Israel inafanya nini mpakani katika eneo la mlima Golan?

Ramani inayoonyesha waliko wanajeshi wa waasi nchini Syria na eneo la Golan Heights ambako Israel imeteka hivi karibuni.
Maelezo ya picha, To request buffer zone: updated 9 Dec1. Complete the translations here: https://tinyurl.com/57kf95xm2. Fill-in the commissioning form https://bit.ly/ws_design_form and this Title in English: Israel creates ‘buffer zone’ near Golan Heights – 2024121003

Waziri mkuu wa Israel ametangaza kuwa vikosi vyake vimeteka eneo lililokuwa na ulinzi mkali mpakani katika mlima Golan- ikipanua maeneo ya Syria yaliyo chini ya Israel.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema hatua hiyo ilikuwa katika hali ya kujilinda hadi pale maafikiano ya uhakika yataafikiwa.

Israel inasema inania ya kuhakikisha hakuna mashambulizi kama yaliyofanyika mwezi Oktoba na Hamas kutoka Syria,anasema Profesa Gilbert Achcar kutoka chuo kikuu cha SOAS.

“lakini hii fursa ni ya kusonga mbele na kuzuia vikosi vingine kusogea karibu na mpaka wa eneo salama.”

Israel kuteka eneo lenye ulinzi mkali mpakani imeshutumiwa vikali na mataifa y akiarabu ,wakitaja hatua hiyo kama kuteka mpaka wa Syria na wanakiuka makubaliano y amwaka 1974 na waziri wa mambo ya nje misiri akisema hayo siku ya Jumatatu.

Ripoti za Syria zinadai kuwa Israel kusogea hadi eneo lililo n aulinzi mkali na pia kufika hadi kilomita 25 Damascus ,lakini Israel imepinga vikali madai hayo.

Vikosi vya usalama vya Israel vimekiri kwa mara ya kwanza kuwa vikosi vyao vinahudumu katika eneo hilo lililona ulinzi mkali katika eneo la mlima Golan,lakini msemaji Nadav Shoshani amesema Israel haijasogea zaidi ya hapo walipofikia.

Je eneo la mlima Golan ni ipi na ni nani anayeutawala?

Golan Heights ni uwanda wa juu wa mawe katika magharibi ya Syria, ambayo imeshikiliwa na Israel kwa zaidi ya nusu karne.

Katika vita vya Mashariki ya Kati vya 1967, Syria iliishambulia Israel kutoka kwenye mwinuko wa Golan, lakini Israel ilirudisha kwa haraka majeshi ya Syria na kuchukua takriban kilomita za mraba 1,200 za eneo hilo, ambalo imekiweka chini ya udhibiti wa kijeshi.

Syria ilijaribu kurudisha eneo la mlima Golan katika vita vya Mashariki ya Kati (vita vya Yom Kippur) vya 1973, lakini ilishindwa.

Nchi zote mbili zilisaini mapatano ya kusitisha mapigano mwaka 1974, na kikosi cha waangalizi wa Umoja wa Mataifa kimekuwa kikiwepo kwenye ushoroba wa kusitisha mapigano tangu mwaka 1974.

Hata hivyo, Israel iliongeza eneo hilo kuwa sehemu yake kisheria mwaka 1981, hatua ambayo haikutambuliwa na wengi katika jumuiya ya kimataifa.

Syria imesema haitakubaliana na makubaliano yoyote ya amani na Israel isipokuwa ifikirie kuondoka kutoka Golan yote.

Wakazi wengi wa Kiarabu wa Golan Heights walikimbia eneo hilo wakati wa vita vya 1967. Hivi sasa, kuna makazi zaidi ya 30 ya Kiyahudi katika eneo la Golan, ambayo yana makazi ya takriban watu 20,000.

Waisraeli walianza kujenga makazi haya mara tu vita vya 1967 vilipomalizika.

Makazi hayo yanadaiwa kuwa yamejengwa kinyume na sheria katika sheria ya kimataifa,lakini Israel haikubaliani na hilo.

Wakaazi wanaishi karibu na raia wa Syria 20,000- wengi wao kutoka jamii ya Druze,ambao hawakukimbia wakati eneo la mlima Golan lilitekwa na Israel.

Je,hofu ya vikosi vya usalama vya Israel vina mashiko?

Wanajeshi wa Israeli wakiweka karibu na uzio wa usalama karibu na kijiji cha Druze cha Majdal Shams, katika Milima ya Golan inayoshikiliwa  na Israeli (8 Desemba 2024)

CHANZO CHA PICHA, EPA

Maelezo ya picha, Gari la jeshi la Israel karibu na Majdal Shams katika milima ya Golan inayotekwa siku ya Jumapili

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema kwamba utawala wa IDF katika eneo la milima ya Golan Heights ni wa muda, lakini kuondoka kwake kunategemea mienendo ya serikali ijayo ya Syria.

“Kama tunaweza kuanzisha uhusiano wa majirani na wa amani na nguvu mpya zinazojitokeza nchini Syria, hiyo ndiyo hamu yetu,” alisema. “Lakini kama hatuwezi, tutafanya kila kinachohitajika kulinda Serikali ya Israel na mipaka yake.”

Dr. HA Hellyer kutoka Taasisi ya Huduma za Kijeshi ya United, taasisi ya think tank iliyoko Uingereza, alisema: “Kilichowajia akilini Waisraeli ni kwamba kuna uwezekano wa uvamizi kutoka kwa vikosi ndani ya Syria na ili kuhakikisha hakuna uwezekano wa hilo, wamejipanga zaidi.”

Hata hivyo, Israel imewahi kushikilia ardhi katika milima ya Golan kama hatua ya kiusalama na kisha kuiimarisha. Inaweza kufanya hivyo tena.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Saar, amesema mashambulizi ya angani dhidi ya vituo vya kijeshi vya Syria yamefanywa tu kwa ajili ya kulinda raia wake.

“Ndio maana tunashambulia mifumo ya silaha za kimkakati kama vile silaha za kemikali zilizobaki au makombora ya umbali mrefu ili zisije zikaangukia mikononi mwa wafuasi wa itikadi kali,” alisema.

Hata hivyo, Prof. Achcar anasema: “Silaha za kemikali hazipo kwa wingi nchini Syria. Zipo tu katika maeneo mawili au matatu. Lakini kwa mashambulizi zaidi ya 300, unajaribu kudhoofisha nchi kabisa.”

Israel ilimtaja Bashar al -Assad kama ”adui waliomjua”anasema,lakini sasa hakuna uhakika ni kipi kitakachofuata.

”Wanatarajia Syria kujigawanya kwa makundi tofauti kama vile Libya,na wanahofia kuwa seriakali itakayoingiamadarakani itakuwa na uhasama zaidi na Israel.

”Wanajipanga kukabiliana na kundi litakalojitokeza na kutumia silaha za Syria dhidi ya Israel.”

picha, Moshi ukifuka kufuatia mashambulizi ya anga mjini Damascus mapema Jumanne asubuhi

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *