Kutoka kuwa kiongozi wa jihadi Syria hadi mwanasiasa muasi: Fahamu Abu Mohammed al-Jawlani alivyoibuka upya
Kiongozi wa waasi nchini Syria Abu Mohammed al-Jawlani ametupilia mbali jina la kivita lililohusishwa na maisha yake ya zamani ya kijihadi, na amekuwa akitumia jina lake halisi, Ahmed al-Sharaa, katika taarifa rasmi zilizotolewa tangu Alhamisi, kabla ya kuangushwa kwa utawala wa Rais Bashar al-Assad.
Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Jawlani za kuimarisha uhalali wake katika muktadha mpya, huku kundi lake la wanamgambo wa Kiislamu, Hayat Tahrir al-Sham (HTS), linaloongoza makundi mengine ya waasi, likitangaza kuuteka mji mkuu wa Syria, Damascus, na kuimarisha udhibiti wake katika sehemu kubwa ya nchi.
Mabadiliko ya Jawlani si ghafla lakini yamekuzwa kwa uangalifu katika kipindi cha miaka mingi, sio tu katika taarifa zake kwa umma na mahojiano na vyombo vya habari vya kimataifa lakini pia katika muonekano wake wa sasa.
Mara baada ya kuvikwa vazi la kitamaduni la wanamgambo wa kijihadi, amechukua mtindo wa Magharibi zaidi katika kipindi cha miaka iliyopita. Sasa, anapoongoza mashambulizi, amevalia kijeshi, kuashiria jukumu lake kama kamanda muongozaji katika chumba cha operesheni.
Lakini Jawlani ni nani – au Ahmed al-Sharaa – na kwa nini na amebadilika?
Uhusiano na IS nchini Iraq
Mahojiano ya PBS ya 2021 na Jawlani yalionyesha kwamba alizaliwa mnamo 1982 huko Saudi Arabia, ambapo baba yake alifanya kazi kama mhandisi wa mafuta hadi 1989.
Katika mwaka huo, familia ya Jawlani ilirudi Syria, ambako alikulia na kuishi katika kitongoji cha Mezzeh huko Damascus.
Safari ya Jawlani kama mwanajihadi ilianza Iraq, ikihusishwa na al-Qaeda kupitia mtangulizi wa kundi la Islamic State (IS) – al-Qaeda nchini Iraq na, baadaye, Islamic State of Iraq (ISI).
Baada ya uvamizi wa Marekani wa 2003, alijiunga na wapiganaji wengine wa kigeni nchini Iraq na, mwaka wa 2005, alifungwa katika gereza la Camp Bucca, ambako aliimarisha uhusiano wake wa kijihadi na baadaye alitambulishwa kwa Abu Bakr al-Baghdadi, mwanazuoni mkimya ambaye baadaye angeendelea kuongoza IS.
Mnamo 2011, Baghdadi alimtuma Jawlani nchini Syria kwa ufadhili wa kuanzisha al-Nusra Front, kikundi cha siri kilichofungamana na ISI. Kufikia mwaka wa 2012, Nusra ilikuwa ni kikosi maarufu cha mapigano cha Syria, kikificha uhusiano wake wa IS na al-Qaeda.
Mvutano uliibuka mwaka 2013 wakati kundi la Baghdadi nchini Iraq lilipotangaza kwa upande mmoja kuunganishwa kwa makundi hayo mawili (ISI na Nusra), na kutangaza kuundwa kwa kundi la Islamic State la Iraq na Waasi (ISIL au ISIS), na kufichua hadharani kwa mara ya kwanza uhusiano huo kati yao.
Jawlani alikataa, kwani alitaka kuwatenganisha kundi lake na mbinu za vurugu za ISI, na kusababisha mgawanyiko.
Ili kutoka katika hali hiyo, Jawlani alitangaza utii kwa al-Qaeda, na kuifanya Nusra Front kuwa tawi lake la nchini Syria.
Tangu mwanzo, alitanguliza uungwaji mkono wa Syria, akijitenga na ukatili wa IS na kusisitiza mtazamo wa kisayansi zaidi wa kijihad.
Kujiunga na al-Qaeda
Mnamo Aprili 2013, al-Nusra Front ikawa mshirika wa al-Qaeda wa Syria, na kuiweka katika mzozo na IS.
Wakati mkakati wa Jawlani ulikuwa kwa kiasi fulani kujaribu kuimarisha uungwaji mkono wa ndani na kuepuka kuwatenganisha Wasyria na makundi ya waasi, muungano wa al-Qaeda hatimaye ulifanya kidogo kufaidi juhudi hii.
Ilikua changamoto kubwa mnamo 2015 wakati Nusra na vikundi vingine vilipoteka mkoa wa Idlib, na kuwalazimisha kushirikiana katika utawala wake.
Mnamo mwaka wa 2016, Jawlani alikata uhusiano na al-Qaeda, na kubadilisha kikundi hicho kuwa Jabhat Fatah al-Sham na baadaye kuwa Hayat Tahrir al-Sham (HTS) mnamo 2017.
Ingawa mwanzoni haikuonekana dhahiri,mgawanyiko huo uliibua tofauti kwa kina.
Al-Qaeda ilimshutumu Jawlani kwa usaliti, na kusababisha uasi na kuunda Hurras al-Din, mshirika mpya wa al-Qaeda nchini Syria, ambayo HTS ililivunja baadaye mwaka wa 2020.
Wanachama wa Hurras al-Din, hata hivyo, wamesalia kuwepo kwa tahadhari katika eneo hilo.
HTS pia ililenga watendaji wa IS na wapiganaji wa kigeni huko Idlib, ikisambaratisha mitandao yao na kuwalazimisha wengine kupitia programu za “dedicalisation”.
Hatua hizi, zilihalalishwa kama juhudi za kuunganisha vikosi vya wanamgambo na kupunguza mapigano, ziliashiria mkakati wa Jawlani kuweka HTS kama mamlaka yenye nguvu kubwa na uwezo wa kisiasa nchini Syria.
Licha ya umma kugawanyika kutoka kuwa al-Qaeda na mabadiliko ya majina, HTS iliendelea kutambuliwa na UN, Marekani, Uingereza na nchi nyingine kama taasisi ya kigaidi, na Marekani ilitangaza zawadi ya $10m kwa mtoa taarifa kuhusu mahali alipo Jawlani.
Mataifa yenye nguvu ya Magharibi yalichukulia mgawanyiko huo kuwa mbinu ya kuhadaa dunia.
Kuunda ‘serikali’ huko Idlib
Chini ya uongozi wa Jawlani, HTS imekuwa jeshi kubwa huko Idlib, kaskazini-magharibi mwa Syria ngome kuu ya waasi na makazi ya takriban watu milioni nne, ambao wengi wao walikuwa wamekimbia kutoka mikoa mingine ya Syria.
Ili kushughulikia wasiwasi kuhusu kundi la wanamgambo linaloongoza eneo hilo, HTS ilianzisha mrengo wa kiraia, kile kinachojulikana kama “Serikali ya ukombozi wa Syria” (SG) mwaka wa 2017 kama tawi lake la kisiasa na kiutawala.
SG ilifanya kazi kama serikali, ikiwa na waziri mkuu, wizara na idara za mitaa zinazosimamia sekta kama vile elimu, afya na ujenzi, huku ikiimarisha baraza la kidini linaloongozwa na Sharia, au sheria ya Kiislamu.
Ili kuunda upya taswira yake, Jawlani alijihusisha kikamilifu na umma, akitembelea kambi za watu waliohama makazi yao, kuhudhuria hafla, na kusimamia juhudi za misaada, haswa wakati wa majanga kama vile matetemeko ya ardhi ya 2023.
HTS iliangazia mafanikio katika utawala na miundombinu ili kuhalalisha sheria yake na kuonyesha uwezo wake wa kutoa uthabiti na huduma.
Hapo awali iliwapongeza Taliban, waliporejea madarakani mwaka 2021, na kuwasifu kama chachu mfano wa kusawazisha juhudi za kijihadi na matarajio ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na kufanya mbinu za maelewano ili kufikia malengo yao.
Juhudi za Jawlani huko Idlib zilionyesha mkakati wake mpana zaidi wa kuonyesha uwezo wa HTS sio tu wa kupigana jihad lakini pia kutawala kwa ufanisi.
Kwa kutoa kipaumbele katika ustawi wa utulivu,taasisi za umma na ujenzi mpya,alilenga kuifanya Idlib kama mfano wa mafanikio chini ya utawala wa HTS,kuyawezesha makundi yote mawili kuhalalisha na kufanikisha matarajio yake kisiasa.
Hata hivyo chini ya uongozi wake HTS imekabiliana na makundi mengine ya wanamgambo yaliyohisi kutengwa,yakiwemo ya kijihadi na ya uasi,ikiwa ni katika jitihada zake za kujiimarisha kimamlaka katika eneo hilo.
Maandamano ya kupinga HTS
Kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya mashambulizi ya waasi yaliyoongozwa na HTS tarehe 27 Novemba, Jawlani alikabiliwa na maandamano huko Idlib kutoka kwa Waislam wenye msimamo mkali pamoja na wanaharakati wa Syria.
Wakosoaji walilinganisha utawala wake na wa Assad, wakishutumu HTS kwa ubabe, kukandamiza upinzani na kuwanyamazisha wakosoaji. Waandamanaji walitaja vikosi vya usalama vya HTS kama “Shabbiha”, neno linalotumika kuwaelezea wafuasi watiifu wa Assad.
Waliendelea kudai kuwa HTS iliekwepa kwa makusudi vita muhimu dhidi ya vikosi vya serikali na kuwatenga wanajihadi na wapiganaji wa kigeni huko Idlib ili kuwazuia kujihusisha na vitendo kama hivyo, yote ili kuwafurahisha mataifa ya magharibi.
Hata wakati wa mashambulizi ya hivi karibuni zaidi, wanaharakati wameendelea kuitaka HTS kuwaachilia huru watu waliofungwa Idlib kwa madai ya kuwa wapinzani.
Katika kujibu ukosoaji huo.HTS ilianzisha mageuzi katika kipindi cha miaka iliyopita.Iliachana na majesho tata yaliyoshutumiwa kukiuka haki za binadamu na kuanzisha idara ya kupokea malalamiko ili kuruhusu raia kufikisha malalamiko yao dhidi ya kundi hilo.
Wakosoaji wake walidai hatua hizi zilikuwa ni kujionyesha tu kwamba inadhibiti wapinzani.
Ili kuhalalisha uimarishaji wake wa mamlaka huko Idlib na usambaratishaji wa makundi ya wapiganaji, HTS iliwataka kuungana chini ya uongozi mmoja ni muhimu kwa ajili ya kuleta maendeleo na hatimaye kupindua serikali ya Syria.
HTS na idara yake ya kiraia, SG, walitumia mbinu ya kujitahidi kuonyesha taswira ya kisasa, ya wastani ili kushawishi raia na jumuiya ya kimataifa,wakati huo huo kudumisha utambulisho wao wa Kiislamu ili kuridhisha watu wenye msimamo mkali ndani ya maeneo yanayoshikiliwa na waasi na HTS wenyewe safu.
Kwa mfano, mnamo Desemba 2023, HTS na SG walikabiliwa na msukosuko baada ya “tamasha” iliyofanyika katika jengo jipya la maduka lilikosolewa na watu wenye msimamo mkali kama “lisilo na maadili”.
Na mwezi huu wa Agosti, hafla iliyoongozwa na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ilileta ukosoaji mkali kutoka kwa watu wenye msimamo mkali, na kusababisha SG kukagua mpangilio wa hafla kama hizo.
Matukio haya yanaonyesha changamoto ambazo HTS inakabiliana nazo katika kupatanisha matarajio ya msingi wa Kiislamu na matakwa mapana ya raia wa Syria, ambao wanatafuta uhuru na kuishi pamoja baada ya miaka mingi ya utawala wa kimabavu chini ya Assad.
Inafuata njia mpya?
Huku tukio la hivi karibuni lilipotokea, vyombo vya habari vya kimataifa viliangazia maisha ya Jawlani ya kijihadi, na kuwafanya baadhi ya wafuasi wa waasi kumtaka arudi nyuma, wakimwona kama anayetumika.
Ingawa hapo awali alionyesha nia ya kufuta kikundi chake na kujiweka kando, vitendo vyake vya hivi karibuni na kuonekana hadharani vinatoa taswira tofauti.
Mafanikio ya HTS katika kuwaunganisha waasi na karibu kuteka nchi nzima katika muda wa wiki mbili yameimarisha msimamo wa Jawlani, kuwatuliza wakosoaji wenye misimamo mikali na shutuma za ubadhirifu.
Jawlani na SG tangu wakati huo wamewahakikishia waangalizi wa ndani na kimataifa.
Kwa raia wa Syria, wakiwemo walio wachache, waliahidi usalama; kwa majirani na mamlaka kama Urusi, waliahidi uhusiano wa amani.
Jawlani aidha aliihakikishia Urusi kwamba ngome zake za Syria hazitadhurika iwapo mashambulizi yatakomeshwa.
Mabadiliko haya yanaonyesha mkakati wa “wanajihadi wenye msimamo wa wastani” HTS tangu 2017.
Mtazamo wa Jawlani unaweza kuashiria kupungua kwa vuguvugu la jihad duniani kama IS na al-Qaeda, ambayo kutobadilika kwao kunazidi kuonekana kuwa siyo endelevu.
Mwenendo wake unaweza kuhamasisha vikundi vingine kubadilika, kuashiria ama enzi mpya ya “jihadi, inayobadilika kisiasa au tofauti ya muda kutoka kwa namna iliyozoeleka kupata mafanikio ya kisiasa na kieneo.