Jay-Z ashtakiwa na Diddy katika kesi ya kumbaka msichana, mwenye umri wa miaka 13, mwaka 2000
Rapa wa Marekani Jay-Z amejibu kesi inayodai kuwa yeye, pamoja na Sean “Diddy” Combs, walimnywesha dawa za kulevya na kumbaka msichana wa miaka 13 kwenye sherehe mwaka 2000.
Mtu ambaye alimshtaki ambaye jina lake halikujulikana anadai alivamiwa kwenye sherehe ya nyumbani baada ya Tuzo za Muziki za Video za MTV (VMAs) huko New York na kwamba mtu mashuhuri wa kike ambaye hakutajwa jina alikuwa kwenye chumba hicho wakati huo.
Katika taarifa yake, Jay-Z, ambaye jina lake halisi ni Shawn Carter, alipuuza hatua hiyo ya kisheria na kusema ni “jaribio la ulaghai”.
Bw Combs, ambaye yuko jela akisubiri kesi yake baada ya kushtakiwa mwezi Septemba kwa biashara ya ngono na makosa mengine, alikanusha shtaka la hivi punde.
Kesi hiyo iliwasilishwa mwezi Oktoba, na iliwasilishwa tena Jumapili ili kuorodhesha Bw Carter kama mshtakiwa.
BBC imewasiliana na wakili wa Bw Carter, Alex Spiro, na mtangazaji wake kwa maoni.
Hatua hiyo ya kisheria iliwasilishwa chini ya sheria ya ulinzi ya waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia ya New York, na wakili wa Texas, Tony Buzbee.
Bw Buzbee amewasilisha kesi kadhaa katika miezi ya hivi karibuni akimtuhumu Bw Combs kwa shambulio na ubakaji. Msanii huyo wa hip-hop anatarajiwa kukabiliwa na kesi ya jinai tarehe 5 Mei.