Kwanini rais wa Korea Kusini alitangaza ghafla sheria za kijeshi?

Kwanini rais wa Korea Kusini alitangaza ghafla sheria za kijeshi?

Rais wa Korea Kusini alishangaza taifa lake usiku wa Jumanne kwa kutangaza ghafla sheria ya kijeshi katika nchi inayojivunia demokrasia kwa mara ya kwanza tangu miaka 50.

Uamuzi wa kushtukiza wa Yoon Suk-yeol – alitangaza usiku katika televisheni ya kitaifa-akitaja hali ya sheria ya kijeshi na tishio kutoka korea Kaskazini.

Lakini ikagunduliwa mapema kuwa nia ya tangazo hilo sio kutokana na tishio kutoka taifa jirani bali ni changamoto zake za kisiasa.

Hata hivyo, iliwasukuma maelfu ya watu kufurika nje ya Bunge la taifa wakiandamana huku wabunge kutoka mrengo wa upinzni wakifika kwa haraka kuidhinisha kura ya dharura ya kuondoa agizo hilo.

Yoon ,baada ya kuzidiwa ujanja alijitokeza dakika chache kukubali kura ya bunge la taifa na kuondoa sheria ya kijeshi aliyoitangaza hapo awali.

Je, ni kipi kilichotokea?

Yoon amekuwa kionekana kama rais aliye na wasiwasi, mchanganuzi anasema.

Katika hotuba yake J umanne usiku ,aliorodhesha majaribio ya upande wa upinzani wake kujaribu kuangusha utawala wake kabla ya kutangaza sheria ya kijeshi ili ”kukabiliana na wakosoaji wake ambao wamekuwa wakihangaisha serikali yake.”

Katika hotuba yake Jumanne usiku,aliorodhesha majaribio ya upande wa upinzani wake kujaribu kuangusha utawala wake kabla ya kutangaza sheria ya kijeshi ili ”kukabiliana na wakosoaji ambao wamekuwa wakihangaisha serikali yake.”

Agizo lake liliweka jeshi kuwake ongoza kwa muda-huku vikosi vya kijeshi na polisi vikitumwa katika jengo la bunge la taifa ambapo helikopta zilionekana zikitua katika paa la jumba hilo.

Vyombo vya habari vilinasa matukio ya vikosi vikiwa vimejihami kwa bunduki vikiingia bungeni huku wafanyakazi wakijaribu kuwazuia kwa kutumia moshi wa vizima moto.

Saa tano usiku za Korea Kusini (saa nane kwa majira ya Afrika mashariki), jeshi liliweka marufuku ya kuandamana na mikutano ya kisiasa na kuweka vyombo vya habari chini ya maagizo ya serikali.

Lakini wanasiasa wa Korea Kusini walitangaza uamuzi wa rais wao ni kinyume cha sheria na ni haramu.

Kiongozi wa chama tawala cha conservative People’s Power Party, pia kilitaja hatua ya Yoon ilikuwa ni ya ”makosa”.

Wakati huo huo kiongozi wa chama cha upinzani cha Liberal Democratic, Lee Jae-myung aliwaagiza kuelekea bungeni kubatilisha uamuzi huo.

Pia aliwarai wananchi wa Korea Kusini kujitokeza kwa wingi kuandamana nje ya Bunge la taifa.

“Vifaru vilivyobeba zana za vita, na maafisa wa usalama wakiwa wamebeba bunduki na visu watatawala nchi yetu….Raia wenzangu nawasihi mjitokeze nje ya bunge la taifa,”

Maelfu waliitikia wito na kukusanyika nje ya bunge la taifa ambaLo lilikuwa limezingirwa na vikosi vya usalama.

Waandamanaji waliimba:”hatutaki sheria ya kijeshi!” na udikteta.”

Vyombo vya habari ambavyo vilikuwa katika maandamano hayo vilinasa video waandamanaji wakivurugana na maafisa wa polisi katika lango la bunge la taifa.

Ingawa sokomoko hiyo haikuzidi na kuwa ya vita,

Wabunge pia walipata fursa ya kupita katika vizuizi vilivyowekwa na polisi- huku wengine wakiamua kuruka juu ya ua ili kufika katika eneo la kupiga kura.

Dakika chache baada ya saa saba usiku ,bunge la Korea Kusini ,wabunge waliokuwa 190 dhidi ya 300 walipiga kura na kubatilisha uamuzi wa rais Yoon uliotajwa sio wa halali.

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol akitangaza sheria ya kijeshi katika hotuba ya kitaifa usiku wa Jumanne

CHANZO CHA PICHA, REUTERS

Maelezo ya picha, Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol akitangaza sheria ya kijeshi katika hotuba ya kitaifa usiku wa Jumanne

Umuhimu wa Sheria ya kijeshi ni upi?

Sheria ya Kijeshi ni utawala wa muda wa mamlaka ya kijeshi wakati wa dharura,ambapo mamlaka ya umma imeonekana kushindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo.

Sheria ya kijeshi iliwahi kutangaza Korea Kusini mwaka 1979,wakati dikteta wa kijeshi wa muda mrefu Park Chung-hee aliuawa wakati wa mapinduzi ya serikali.

Haijawahi kutangazwa tena tangu demokrasia kupitia bunge ianzishwe mwaka 1987.

Lakini Jumanne,Yoon alipasua mbarika na kuitangaza akitaja ni njia ya kujihami dhidi ya mahasimu wa nchi hiyo.

Yoon, ambaye amechukua uamuzi mkali dhidi ya Korea Kusini tofauti na watangulizi wake ,amedokeza kuwa chama cha upinzani kinashirikiana na Korea Kaskazini ilhali hana ushahidi wowote.

Katika sheria ya kijeshi,mamlaka zaidi hupatiwa wanajeshi na mara nyingi haki za umma ,sheria na hifadhi zake hutupiliwa mbali.

Ingawa jeshi ilipiga marufuku ya shughuli za kisiasa na uanahabari kufanyika- waandamanaji na wanasiasa walipuuza agizo hilo.

Na hakukuonekana serikali ikijaribu kuzuia wanahabari kuendelea na shughuli za kutangaza matukio ya wakati huo -kituo cha kitaifa cha matangazo Yonhap na vyombo vya habari viliendelea kupeperusha taarifa kama kawaida.

 Bunge la Korea Kusini lilikutana dakika chache baada ya tangazo la Yoon ili kubatilisha sheria ya kijeshi

CHANZO CHA PICHA, REUTERS

Maelezo ya picha, Bunge la Korea Kusini lilikutana dakika chache baada ya tangazo la Yoon ili kubatilisha sheria ya kijeshi

Ni kipi kilichompa jakamoyo rais Yoon?

Yoon alichaguliwa madarakani mwezi Mei 2022 kama kiongozi sugu wa Conservative, lakini amekuwa amepoa sana kama rais tangu mwezi Aprili wakati upande wa upinzani ulishinda katika uchaguzi mkuu.

Serikali yake haijaweza kupitisha mswada wowote bungeni, walioutaka na imekuwa ni uwanja wa Upinzani chama cha Liberal kuamua mswada wa kuidhinisha.

Vile vile,umaarufu wake umeshuka hadi asilimia 17 kutokana na kashfa za ufisadi mwaka huu ikiwemo ile ya mke wa rais kupokea zawadi ya mkoba wa kifahari na masuala mengine ya kutumia vibaya mamlaka.

Mwezi mmoja tu uliopita, alilazimika kutoa pole kwa umma kupitia televisheni ya kitaifa, akisema alikuwa anabuni ofisi ya kusimamia majukumu ya mke wa Rais.

Hata hivyo, alikataa wito wa uchunguzi ambao vyama vya upinzani vilikuwa vikiiitaka.

Mapema wiki hii, upinzani uliwasilisha pendekezo la kupunguza mgao mkubwa wa bajeti ya serikali ambao hauwezi kupingwa.

Wakati huo huo, upinzani pia ulianzisha mchakato wa kuwang’oa mawaziri na mawakili wakuu kadhaa – akiwemo Mkuu wa Shirika la Ukaguzi la serikali – kwa kushindwa kuchunguza shughuli za Mke wa Rais.

Raia wengi walikusanyika nje y abunge la tiafa usiku wa Jumanne dhidi ya sheria ya kijeshi .Maandamano ya kisiasa yamekuwa ya kawaida nchini humo.

CHANZO CHA PICHA, REUTERS

Maelezo ya picha, Raia wengi walikusanyika nje y abunge la tiafa usiku wa Jumanne dhidi ya sheria ya kijeshi .Maandamano ya kisiasa yamekuwa ya kawaida nchini humo.

Kiongozi wa upinzani akihutubia wanahabari baada ya wabunge kutupilia mbali sheria ya kijeshi

CHANZO CHA PICHA, REUTERS

Maelezo ya picha, Kiongozi wa upinzani akihutubia wanahabari baada ya wabunge kutupilia mbali sheria ya kijesh

Ni kipi kitakachofuata?

Tangazo la Yoon lilishangaza wengi na kwa kipindi cha saa sita, Wakorea Kusini walikuwa katika hali ya taharuki kuhusu maana ya amri ya sheria ya kijeshi.

Lakini upinzani ulikusanyika haraka bungeni na ulikuwa na idadi ya kutosha kupinga tangazo hilo.

Licha ya kuwepo kwa jeshi na polisi kwa wingi katika mji mkuu, inaonekana kwamba mapinduzi ya kijeshi hayajatokea.

Kwa mujibu wa sheria za Korea Kusini, serikali lazima ifute sheria ya kijeshi ikiwa bunge litaamua kwa wingi kupiga kura.

Sheria hiyo hiyo inakataza mamlaka ya sheria ya kijeshi kuwakamata wabunge.

Hali ya sasa bado haijajulikana na ni vigumu kusema madhara yatakayojitokeza kwa Yoon.

Baadhi ya waandamanaji waliojitokeza nje ya bunge jioni ya Jumanne walikuwa wakipiga kelele: “Mkamate Yoon Suk-yeol”. Lakini hatua yake ya ghafla imewashtua kwa hakika wananchi wa nchi hii, ambao wanajivunia kuwa na demokrasia inayostawi na inayoendelea tangu siku za utawala wa kidikteta.

Hii inachukuliwa kama changamoto kubwa zaidi kwa jamii hiyo ya kidemokrasia katika miongo kadhaa.

Wataalamu wanakisia kuwa inaweza kuwa na madhara makubwa zaidi kwa sifa ya Korea Kusini kama demokrasia kuliko hata maandamano ya Januari 6 huko Marekani.

“Tangazo la Yoon la sheria ya kijeshi linaonekana kama matumizi ya nguvu za kisheria kupita kiasi na makosa ya kisiasa, likiweka hatarini uchumi na usalama wa Korea Kusini,” alisema mtaalamu, Leif-Eric Easley kutoka Chuo Kikuu cha Ewha huko Seoul.

“Alionekana kama mwanasiasa aliyejaa shinikizo, akifanya haraka hatua dhidi ya kashfa zinazozidi kuongezeka, upinzani wa kimaashtaka na wito wa kumng’oa, ambayo sasa ni wazi yatakuwa na nguvu zaidi.”

Kama alivyosema spika wa bunge Jumatano: “Tutailinda demokrasia pamoja na watu”.

picha, Polisi wakishika doria katika lango la bunge la taifa la Korea kaskazini baada ya rais wa nchi hiyo kutangaza sheria ya kijeshi

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *