Je, rais wa Korea Kusini aliyetangaza amri ya kijeshi anayekumbwa na kashfa ni nani?

Je, rais wa Korea Kusini aliyetangaza amri ya kijeshi anayekumbwa na kashfa ni nani?

Mustakabali wa rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol uko njia panda baada ya usiku wa machafuko ambapo alitangaza sheria ya kijeshi na kisha kuiondoa ghafla, na kuitumbukiza nchi hiyo katika machafuko.

Yoon, ambaye alishinda urais kwa kura chache 2022, hakupendwa sana na Wakorea Kusini na amekuwa akikabiliwa na shinikizo tangu ashindwe uchaguzi wa bunge mnamo Aprili, huku hatua hiyo ikionekana kuwa sawa na kura ya kutokuwa na imani naye.

Pia amekumbwa na matatizo binafsi. Mwezi uliopita aliomba msamaha katika hotuba yake kwa taifa kwa msururu wa mabishano yaliyomzunguka mkewe ambayo ni pamoja na madai ya kukubali mkoba zawadi ya kifahari ya mkoba wa Dior na udanganyifu wa hisa.

Sasa anakabiliwa na madai ya kujiuzulu na wabunge wamesema watamng’oa madarakani.

Jaribio la usiku wa Jumanne la kuweka sheria ya kijeshi lilimshangaza kila mtu.

Iliwafanya wabunge katika bunge la taifa mjini Seoul kupiga kura dhidi ya amri hiyo. Nje, polisi walikuwa wamekusanyika wakati maelfu ya waandamanaji walikusanyika kwa hasira.

Umati huo huo ulipiga kelele za shangwe wakati Yoon aliporejea ndani saa kadhaa na kutangaza kuwa ataondoa amri ya sheria ya kijeshi.

Hatua yake ya kuweka sheria kali, na kisha kurudi kuibatilisha , iliwashanga za Wakorea Kusini na ulimwengu wote.

Unaweza pia kusoma:

Kupanda mamlaka

Yoon alikuwa mgeni katika siasa wakati aliposhinda urais. Alijizolea umaarufu wa kitaifa kwa kufungua kesi ya ufisadi dhidi ya rais wa zamani Park Geun-hye mwaka 2016.

Mnamo 2022, mwanasiasa huyu mpya alimshinda mpinzani wake wa kiliberali Lee Jae-myung kwa chini ya 1% ya kura – matokeo ya karibu zaidi ambayo nchi hiyo imemewahi kuyashuhudia tangu uchaguzi wa moja kwa moja ulipoanza kufanyika mnamo 1987.

Wakati ambapo jamii ya Korea Kusini ilikuwa ikikabiliana na mgawanyiko mkubwa juu ya masuala ya kijinsia, Yoon aliwavutia wapiga kura vijana wa kiume kwa kupinga ubaguzi wa kijinsia.

Watu walikuwa na “matumaini makubwa” kwa Yoon wakati alipochaguliwa, alisema Don S Lee, profesa mshiriki wa utawala wa umma katika chuo kikuu cha Sungkyunkwan. “Wale waliompigia kura Yoon waliamini kwamba serikali mpya chini yake itafuata maadili kama kanuni, uwazi na ufanisi.”

Yoon pia ametetea msimamo wa kuongeza riba katika biashara na Korea Kaskazini. Taifa hilo la kikomyunisti lilitajwa na Yoon Jumanne usiku wakati alipojaribu kuweka sheria ya kijeshi.

Alisema anahitaji kulinda nchi dhidi ya vikosi vya Korea Kaskazini na “kuondoa vipengele vya kupambana na serikali”, ingawa ilikuwa dhahiri tangu mwanzo kwamba tangazo lake lilitokana na tisho kutoka Kaskazini na zaidi lilihusu matatizo yake ya ndani.

Yoon anajulikana kwa kufanya makosa kisiasa , ambayo hayakumsaidia. Wakati wa kampeni yake ya 2022 ilibidi abadilishe usemi wake kwamba rais wa kiimla Chun Doo-hwan, ambaye alitangaza sheria ya kijeshi kusababisha maandamano makubwa mnamo 1980, alikuwa “mzuri katika siasa”.

Baadaye mwaka huo alilazimika kukana kulitukana bunge la Marekani katika matamshi yaliyotolewa baada ya kukutana na rais wa Marekani Joe Biden mjini New York.

Alinaswa kwenye kipaza sauti na kuonekana kwenye kamera akiwaita wabunge wa Marekani neno la Kikorea ambalo linaweza kutafsiriwa kama “wapumbavu” au kitu tusi baya zaidi. Video hiyo ilisambaa kwa kasi nchini Korea Kusini.

Yoon amekuwa na mafanikio katika sera za kigeni, hasa katika kuboresha uhusiano wa kihistoria wa nchi yake na Japan.

‘Upotoshaji wa kisiasa’

Urais wa Yoon umekumbwa na kashfa, nyingi zikijikita kati yake na mke wake Kim Keon Hee, ambaye alituhumiwa kwa ufisadi na ushawishi wa ulanguzi – hasa akidaiwa kupokea kifurushi cha Dior kutoka kwa mchungaji.

Mnamo Novemba, Yoon aliomba msamaha kwa niaba ya mkewe wakati akikataa wito wa kuhusu shughuli zake.

Lakini umaarufu wake wa urais ulibaki kuwa wa kushangaza. Mapema mwezi Novemba, kiwango chake cha kukubalika kilishuka hadi asilimia 17, rekodi ambayo ni ya chini tangu alipoingia madarakani.

Mwezi Aprili, chama cha upinzani cha Democratic kilishinda uchaguzi wa bunge kwa kishindo, na kusababisha kushindwa kwa Yoon na chama chake cha People Power.

Yoon alishushwa hadhi na kuwa rais asiye maarufu na kuwa rais anayeidhinisha miswada ya kura ya turufu iliyopitishwa na upinzani, mbinu ambayo aliitumia kwa “kiwango ambacho hakikutarajiwa kawaida”, alisema Celeste Arrington, mkurugenzi wa taasisi ya chuo kikuu cha George Washington cha mafunzo ya Kikorea.

Wiki hii, upinzani ulipunguza bajeti ambayo serikali na chama tawala walikuwa wameiweka – na muswada wa bajeti hauwezi kupingwa.

Wakati huo huo, upinzani ulikuwa unaelekea kuwashtaki mawaziri, hasa mkuu wa idara ya ukaguzi wa serikali, kwa kushindwa kumchunguza mke wa rais.

Huku akikabiliwa na changamoto za kisiasa, Yoon aliamua chaguo la nyuklia – hatua ambayo wachache, ikiwa ipo, wangeweza kuitabiri.

“Waangalizi wengi wana wasiwasi katika wiki za hivi karibuni kuhusu mgogoro wa kisiasa kwasababu ya makabiliano kati ya rais na bunge la taifa linalodhibitiwa na upinzani,” alisema Dkt Arrington, “ingawa wachache walitabiri hatua kali kama hiyo kama kutangaza sheria ya kijeshi.”

Tangazo la Rais Yoon la sheria ya kijeshi lilikuwa “ukiukaji wa sheria na hesabu ya kisiasa”, kulingana na Leif-Eric Easley, profesa wa masomo ya kimataifa katika chuo kikuu cha Ewha Womans huko Seoul.

“Kwa msaada mdogo sana wa umma na bila kuungwa mkono na nguvu ndani ya chama chake na utawala, rais anapaswa kujua jinsi ingekuwa vigumu kutekeleza amri yake ya usiku wa manane,” Dr Easley aliiambia BBC.

“Alisikika kama mwanasiasa aliyezingirwa, akichukua hatua ya kukata tamaa dhidi ya kashfa zinazoongezeka, vizuizi vya taasisi, na wito wa kuondolewa madarakani, yote ambayo sasa yanaweza kuongezeka.”

h

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Jumatano asubuhi raia wa Korea Kusini waliibuka kutoka moja ya usiku wa ghasia zaidi katika kumbukumbu ya hivi karibuni

Nini kinachoendelea sasa?

Yoon amevutia hisia kutoka kwa wanasiasa wa pande zote mbili, wakati wabunge walipokusanyika kwa haraka – wakiwemo baadhi kutoka chama cha Yoon – walipopiga kura ya kuondoa sheria ya kijeshi Jumanne usiku. Chama cha upinzani cha Democratic kinajaribu kumng’oa madarakani Yoon, na hata uongozi wa chama cha Yoon umetaka rais huyo kujiondoa katika chama hicho.

Wasaidizi wakuu wa Yoon walijitolea kujiuzulu siku ya Jumatano, shirika la habari la Yonhap liliripoti.

Kiongozi wa upinzani Lee anatabiri matumaini, akiwaambia waandishi wa habari kwamba “tangazo haramu la sheria ya kijeshi” ni “fursa ya kuamua kuvunja uongozi mbaya na kurudi katika jamii ya kawaida”.

Matokeo ya Jumanne usiku yanatarajiwa kuwa na athari nje ya mipaka ya Korea Kusini. Tangazo la Yoon limewakasirisha washirika wa Korea Kusini. Maafisa nchini Marekani, mshirika muhimu, wamesema kuwa hawakutarajia tangazo la Yoon, na wanaitaka Korea Kusini kutatua mzozo huo “kwa mujibu wa utawala wa sheria”.

Japan inasema inafuatilia hali ya Korea Kusini kwa “wasiwasi wa kipekee na mkubwa”.

Wakati huo huo, Korea Kaskazini, ambayo imezidisha mvutano na Kusini katika miezi ya hivi karibuni, inaweza “kujaribu kutumia mgawanyiko huko Seoul,” alisema Dk Easley.

Hasira bado inaendelea kuikumba Korea Kusini. Siku ya Jumatano waandamanaji walimiminika mitaani wakimlaani Yoon. Moja ya vyama vikubwa vya wafanyakazi nchini humo vyenye wanachama zaidi ya milioni moja kinatoa wito kwa wafanyakazi kuendelea na mgomo hadi atakapojiuzulu.

Haijulikani ni nini Yoon anapanga kufanya. Bado hajaonekana hadharani tangu fiasco.

“Kwa muda mrefu amekuwa akilaumiwa kutokana na jinsi alivyoshughulikia matatizo ambayo yameibuliwa na mwenendo wake na mwenendo wa mke wa rais,” waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Korea Kusini Kang Kyung-wha alikiambia kipindi cha BBC Newsday. “Jukumu ni la rais kutafuta njia ya kutoka kwenye kona hii ambayo amejiweka ndani.”

Lakini bila kujali jinsi Yoon atakavyojiondoa katika mzozo huu, tamko lake la sheria ya kijeshi linaweza ni njia yake ya kuumaliza urais wake usio na mamlak.

picha, Tangazo la rais wa Korea Kusini la sheria ya kijeshi limekuja kama mshangao kwa raia wa Korea Kusini na dunia nzima

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *