Tetesi za soka Ulaya: Mohamed Salah analengwa na klabu za Saudia

Tetesi za soka Ulaya: Mohamed Salah analengwa na klabu za Saudia

Winga wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 32, ndiye ‘ndoto’ ya usajili wa Saudi Pro League msimu ujao. (Mail – Subscription Required)

Manchester United wanapanga uhamisho wa pauni milioni 50 ili kuwashinda Chelsea kwa ajili ya kumnunua beki wa kati wa Benfica na Ureno Tomas Araujo, 22, mwezi Januari. (Sun),

Beki wa Crystal Palace, 24, Muingereza, Marc Guehi, anatamani kujiunga tena na Chelsea, wakati Newcastle pia bado wanavutiwa na beki huyo wa kati. (TeamTalks)

Hatua ya Arsenal ya kutaka mshambuliaji mpya imepata pigo kwa Viktor Gyokeres, 26, anayetaka kumfuata meneja wa zamani wa Sporting Lisbon Ruben Amorim kwenda Manchester United. (Football.London).

.GETTY IMAGES, Mshambuliaji wa Sporting Lisbon Gyokeres

The Gunners wana takriban washambuliaji sita kwenye orodha ya wachezaji inaowalenga , akiwemo mshambuliaji wa Newcastle United na Uswidi Alexander Isak, 25. (Caught Offside)

Manchester City na Manchester United wamepewa fursa ya kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 26, na kiungo wa kati wa Italia na Juventus Fagioli, 23, . (Gazzetta dello Sport – In Itali)

Meneja wa Chelsea Enzo Maresca amekanusha kuwa Christopher Nkunku anauzwa, licha ya fowadi huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27 kuwa na muda mfupi wa kucheza. (Times – Subnscription Required)

. Almiron

Fowadi wa Paraguay Miguel Almiron, 30, ataruhusiwa kuondoka Newcastle mwezi Januari. (Telegraph – Subscription Required),

Manchester City pia inamfuatilia kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach Mjerumani Rocco Reitz mwenye umri wa miaka 22 juu ya uwezekano wa kuhama mwezi Januari. (GiveMeSport), nje

Napoli wameiuliza Arsenal kuhusu upatikanaji wa beki wa Poland Jakub Kiwior, 24, kwa mkopo mwezi Januari. (Gianluca di Marzio, via Metro),

Ufitinema Aime Gerard

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *