Maana zilizofichika katika mchoro wa utupu wa karne ya 16
Mchoro ambao ni nadra kuonekana wa Raphael’s The Three Graces umedhihirisha dhana ya enzi hizo kuhusu uchi,ustaarabu,aibu – na kipaji cha msanii.
Ni sehemu ya maonyesho, Kuchora kipindi mwamko-sanaa cha kiitaliano-kwenye Jumba la sanaa la Mfalme, kasri la Buckingham – la michoro kutoka 1450 hadi 1600, kubwa zaidi ya aina yake kuwahi kuonyeshwa nchini Uingereza.
Kambamti anayetangatanga na mbuni shupavu kati ya michoro 150 ya chaki, sehemu ya chuma na wino kwenye maonyesho ya Kuchora Mwamko wa Kiitaliano, kwenye Jumba la sanaa la Mfalme, kasri ya Buckingham. Iliyoundwa na wasanii maarufu kama vile Leonardo da Vinci, Michelangelo, Raphael na Titian, ilijumuishwa katika Mkusanyiko wa Kifalme katika Karne ya 17 chini ya Mfalme Charles II, kama zawadi.
Kati ya michoro 30 zaidi, ni mara yao ya kwanza kuonyeshwa hadharani. Ingawa michoro hii ilikuwa nadra kuonyeshwa kutokana na uharibifu wake, leo inatambulika kama sanaa. Maonyesho haya ni sehemu ya maonyesho mapana ya michoro ya Italia kutoka 1450 hadi 1600 zilizowahi kuonyeshwa Uingereza.
Michoro ya uchi wa kike ni adimu zaidi kuliko tafiti hizi za wanyama, zikizidiwa kwa idadi ya watu watatu na wingi wa wanaume uchi.
“Mwili wa kiume ni lengo hili kamili la ubunifu,” alielezea mwanahistoria wa mwamko sanaa Maya Corry, akijadili maonyesho kwenye idhaa ya BBC Radio 4 mwezi Oktoba.
“Hii ni jumuiya ya Kikristo na ni mwili wa kiume, si mwili wa kike, ambao umeumbwa kwa mfano wa Mungu.” Vitruvian Man ya Leonardo Da Vinci, na uwiano wake bora wa mwili, ni mfano wa uhakika. Ni umbile la kiume, alisema, ambalo “hukaribia zaidi ukamilifu wa kimungu” katika nyakati hizo.
Kulikuwa na masuala ya kijamii pia. “Warsha ya msanii ingekuwa mazingira ya kiume, na bila ya kuwepo kwa mwanamitindo mzoefu ingekuwa imekwenda kinyume na kanuni zote za kijamii kwa mwanamke kuvua nguo mbele ya mwanamume yeyote isipokuwa mumewe,” Martin Clayton, msimamizi wa maonyesho. , anaiambia BBC.
Ilikuwa ni mifano ya kiume ambayo ingejitokeza kwa Michelangelo, kwa mfano, wakati alihitaji takwimu ya kike. “Hii ilisababisha kutoelewana na upotoshaji katika taswira ya mwili wa kike.”
Raphael, hata hivyo, alikuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza kukubaliana na mtindo huo, akichora uchi wa kike kulingana na mifano ya maisha halisi.
“Alikuwa msanii mwenye ujuzi wa hali ya juu, ambaye alitumia kuchora kwa ustadi kutatua shida za kuona, na kufanya kazi haraka sana kutoka kwa wazo la kwanza hadi utunzi wa mwisho,” anasema Clayton. Michoro “inaturuhusu kuona majibu ya haraka ya msanii kwa takwimu hai walipokuwa wakichunguza picha, uwiano, harakati na maelezo ya kimaumbile,” anaongeza.
Kwa upande wa Raphael, “uamuzi wake kwa wakati mmoja na uwazi kwa tofauti na uwezekano daima huonyeshwa.”
Picha ya The Three Graces ya Raphael (c1517-18), iliyochorwa kwa chaki nyekundu na baadhi ya michoro ya chuma, inaonyesha ubunifu wa msanii.
Akitumia mfano mmoja katika mikao mitatu tofauti, tunashuhudia mchakato wa uchoraji uliopelekea kuundwa kwa fresko maarufu The Wedding Feast of Cupid and Psyche, ambapo hawa wanawake watatu watakuwa sehemu muhimu ya sherehe ya harusi, wakibariki furaha ya wanandoa wapya.
Uchi wa wanawake hawa ni kipimo cha ufanisi wa msanii wa mwamko sanaa , na pia unaridhisha hamu ya kipindi hicho kuhusu sayansi.
Misuli ya mabega na mguu wa wanawake inaonyesha umuhimu wa umbile , kama vile picha maarufu The Muscles of the Leg ya Da Vinci (c1510-11), pia iliyoonyeshwa.
Hata hivyo, kuna upole zaidi katika uso na tumbo la wanawake hawa, tofauti na picha za wanaume kwenye maonyesho, kama The Head of a Youth(c1590) inayohusishwa na Pietro Faccini, au St Jerome (c1580) ya Bartolomeo Passarotti, ambazo zinaonyesha sura ngumu na misuli ya nguvu.
Dhana ya jinsia ya kike
Kama ilivyokuwa kwa David wa Michelangelo, ambaye alichora picha miaka kumi kabla, Raphael alionyesha sura bora, hata alipokuwa akichora kutoka kwa maisha halisi.
Katika barua aliyomwandikia rafiki yake Baldassare Castiglione mwaka 1514, alielezea changamoto ya kupata ukamilifu katika uchoraji wa wanawake.
Alisema: “Ili kumchora mwanamke mrembo, nitalazimika kuona warembo kadhaa. Lakini kwa kuwa wanawake warembo ni wachache, mimi hutumia wazo fulani linalokuja akilini.”
Katika picha ya The Three Graces ya Raphael, “uzuri” unamaanisha ngozi laini, isiyo na doa, na maumbile ya mwili kama vile matiti na makalio yaliyo duara, sawa na tufaha. Sandro Botticelli alionyesha uzuri wa kike katika picha yake maarufu Spring, kwa kutumia nywele zinazotiririka na vitambaa, huku picha ya Pietro Liberi kutoka mwishoni mwa mwamko sanaa (c1670-80) ikisisitiza uso mzuri na mwili wa marumaru.
Picha hizi pia zinapatikana katika michoro kama The Head of the Virgin ya Federico Barocci (c1582), ilichora karne moja baadaye.
“The Three Graces” zinaweza kuwa ziliunda sehemu ya safu ya ‘uchi mzuri’, ambapo uchi ulikuwa ishara ya ukweli na usafi wakati mwingine ulihusishwa na aibu kama anavyosema Julia Biggs.
Upungufu wa wanawake wachoraji na wasimamizi wa sanaa katika kipindi cha mwamko sanaa ulifanya picha nyingi kuonyeshwa kupitia macho ya kiume.
Julia Biggs, mtaalamu wa historia ya sanaa ya mwamko, anasema: “Mtazamo wa jinsia na nafasi ya chini ya wanawake katika jamii ya mwamko sanaa ulionyeshwa katika picha, ambapo wanaume walionyesha hadhi yao ya kijamii, kisiasa, au kitaaluma.
Kinyume chake, wanawake walisawiriwa hasa kuhusiana na sifa za uzuri wa kike (ujana), utu wema (adabu, unyenyekevu, utii), na maumbile ya kike.”
The Three Graces (Euphrosyne, Aglaea, na Thalia), binti za Mungu Zeus katika kisasili cha Kigiriki, ni picha zinazofanywa kwa umaridadi na uzuri wa kipekee.
Katika uchoraji wa Raphael, picha hizi zinawakilisha mtazamo wa kiume kuhusu jinsi mwanamke anapaswa kuonekana na tabia anazopaswa kuwa nazo. Michoro hii inajumuisha dhana ya The Graces, ambayo inaashiria uzuri, wema, na upendo.
Dansi ya duara ya Graces inasisitiza usawa na umoja, kanuni kuu za urembo wa mwamko sanaa. Kama kundi, wanachanganya maadili ya uzuri wa kike na, bila kutarajia, wanasherehekea umbo la kike na uhusiano wa kike.
Wakati huo, uchi wa kike ulikuwa na maana tofauti.
Kwa upande mmoja, Biggs anasema kwamba The Three Graces huenda ziliwakilisha “uchi wa wema,” ambapo uchi ulikuwa ishara ya ukweli na usafi.
Hata hivyo, uchi wa kike pia ulionyeshwa kama ishara ya aibu. Kwa mfano, katika picha maarufu ya Expulsion from the Garden of Eden (c1424-27), Hawa pekee anafunikwa sehemu za siri, kama aliyetajwa kuwa mwenye dhambi.
Biggs anasisitiza pia kwamba katika baadhi ya maeneo, kama Ferrara, Italia, wanawake walifanywa kutembea uchi kama sehemu ya dhihaka ya kijamii, inayoitwa la scopa.
Uchi wa kike katika usanii wa mwamko sanaa ulikuwa tofauti na kanuni za mavazi ya kike za kipindi hicho, hasa nchini Italia.
Biggs anasema kwamba, hadharani, wanawake walifunika miili yao kuanzia chini ya shingo hadi miguu na mikono yao. Hata hivyo, hadithi za Biblia na za kihekaya ziliwapa wasanii nafasi ya kuonyesha wanawake bila mavazi.
Biggs anaongeza kwamba wanaume waliokuwa wasimamizi wa sanaa walitaka kuonyesha nguvu zao za kijinsia kupitia michoro hii.
Pamoja na hayo, hata wanawake walipovaa mavazi, michoro ya Kuchora Mwamko wa Kiitaliano ilionyesha majukumu tofauti waliyokuwa nayo, kama vile seductress (mwanamke mrembo anayeongoza) katika picha ya Annibale Carracci ya The Temptation of St. Anthony (c1595), au Bikira Maria kama ilivyokuwa katika michoro ya Michelangelo na Da Vinci.
Hata hivyo, maonyesho haya yanatufundisha zaidi ya kusimama tu mbele ya picha; yanatufanya tushiriki kwa ubunifu wetu. Kwa baadhi ya fursa, tunapata nafasi ya kurekebisha na kuelewa upya picha za mwanamume na mwanamke katika sanaa.